HATUPIMI BANDO

27 July 2013

GOOGLE YAOMBA USHIRIKIANO NA CHEKA NA KITIME


Mambo yamepamba moto Bongo, baada ya dada yetu mpenzi kukubaliwa na JLO kufanya kolabo, milango ghafla imefunguka kwa nyanja nyingi za Wabongo. Klabu zetu za soka kubwa  Kandambili na Mnyama zimeingizwa ligi kuu ya Uingereza, klabu hizi maarufu zinategemewa kuleta upinzani mkubwa utakayoweza kuleta hamasa kubwa zaidi katika ligi hii maarufu. Madereva watatu wa bodaboda toka Iringa wamechaguliwa kushiriki katika mashindano ya pikipiki ya Grand Prix, hii imekuja baada ya sifa za madereva wa Bodaboda kuvuka mipaka ya nchi yetu changa. Wakati huohuo  waendesha baiskeli wawili toka jiji la Mwanza wamo katika orodha ya waendesha baiskeli watakaoenda kuchuana na wenzao wa Ufaransa katika mashindano ya baiskeli ya Tour De France.  Na huko Holywood filamu tatu zimepeleka maombi Bongomovies ili kupata ushauri kuhusu taaluma ya uigizaji na ikiwezekana kupata waigizaji watakaoweza kuinua tena biashara ya filamu ambayo imeanza kudorora, mambo haya yote kwa ujumla yamepandisha sana chati nchi yetu. Hata blog hii nayo imeteuliwa kuwemo katika bodi ya washauri wa kampuni ya Google.

No comments: