PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

CHEKANAKITIME BLOG YAFUNGUA KAMPUNI YA BIASHARA ZA KIMATAIFA

Baada ya kila jitihada kupata matangazo katika blog hii kukwama, blog hii imegundua biashara mpya kabisa ambayo itasaidia kuingizia blog hii fedha nyingi zikiwemo fedha za kigeni. Wakurugenzi walioishiwa mkwanja wa blog hii wamefungua kampuni ambayo imeamua kujikita katika kurekebisha makosa ambayo yamefanyika katika miili ya wadada.
Wadada wengi wamekuwa na tabia ya kujichora tatoo na baada ya muda kugundua kuwa hawazitaki, hivyo blog hii imejikita katika biashara ya kuondoa tatoo. Kwa kutumia teknlojia inayoitwa Tatuu Rimuva wamejipanga kuondoa tatoo kwa mfano zilizopo hapo chini. Meneja masoko ametumwa kuwatafuta wenye tatuu hizi na kujaribu kuingia nao katika mkataba huu mnono wa kuondoa tatuu zao kwa machine iliyopo hapo juu. Tayari wafanya kazi sita wamemaliza kozi ya digrii ya kutumia mashine hiyo mpya.

Comments