PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BREAKING NYEUSSSSSSSSSSS.....MEN IN BLACK 4 KUTENGENEZWA TANZANIA

Waandishi ngangari wa blog hii wagundua kitu ambacho kinaendeshwa kwa siri sana, lakini kama mitihani ya fom fo nacho kimeliki. Mradi mkubwa wa kutengeneza filamu ya MEN IN BLACK 4 utafanyika Bongo na wahusika wamekwisha teuliwa.
Jamaa hao ambao tayari wameanza mazoezi ya kuvaa suti nyeusi kama Will Smith na Tommy Lee Jones wananvyofanya, wameonekana Kawe wakifanya mazoezi katika sehemu siri sana pale kwenye hoteli karibu na raundabaut ya Kawe.  Hii siri imefichuliwa na waandishi wetu kwa kutumia utaalamu wa hali ya juu sana, si vizuri kuieneza.

Comments