PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BOSI KWANI WEWE UNATAKA IWE NGAPI?

Kulikuwa na tangazo la kazi, watu watatu, mwanafuzi, mhasibu na mwanasiasa wakapeleka maombi, siku ya usaili wakafika tayari kwa usaili;
MSAILI: Je 2+2 ni ngapi?
MWANAFUNZI: 4
MSAILI: Haya nenda niitie mwenzio
MSAILI: Je, 2+2 ni ngapi?
MHASIBU: Kwa ujumla ni 4, inaweza ikazidi kidogo au kupungua kidogo kwa asilimia kama 10 hivi lakini ni 4
MSAILI: Duh haya nenda niitie mwenzio
MSAILI: Je 2+2 ni ngapi?
MWANASIASA: Kitu kikubwa hapa ni kuangalia trend ya wapiga kura, haya mambo unaweza ukajibu kwa harakaharaka ukakuta mambo yamebadilika yakakukosti kwenye uchaguzi. Kimsingi kwanza ni muhimu kujua msimamo NA muelekeo wa Chama chako, na pia kuangalia je jibu lako  lina matokeo gani katika muktadha mzima wa swala lenyewe.
MSAILI: Hebu jibu swali 2+2 ni ngapi?
MWANASIASA:(Kwa sauti ya chini) We unataka iwe ngapi bosi?

Comments

Anonymous said…
Kitime, si tu unachuvunja mbavu, utatuuwa baba!.
Asante sana.