PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BLOG YAANZISHA TIMU YA SOKA YA KIMATAIFA, LIGI ZA UINGEREZA NA SPAIN TUMBO MOTO

Katika kile ambacho kimekuwa gumzo kubwa katika anga la Kimataifa la soka, Blog yenu ya Cheknakitime imeanzisha timu kali sana ya soka. Timu hii ambayo jopo la wataalamu wasio na taaluma wamesema itakuwa tishio kwa timu kama Arsenal, Manchester United, Manchester City na hata Barcelona za Buguruni. Golikipa wa timu hii(anaonekana pichani), amenunuliwa kwa fedha nyingi ambazo hazitatajwa hapa ili watu wasimfuate fuate kumuomba bia mwezi huu.
Timu nyingi zimeanza safari za kwenda kwa masangoma ili kuvunja nguvu za timu hii ambayo kama haitazuiliwa lazima hatimae itacheza kombe la dunia.
Mazoezi ya timu hii ni ya siri sana yanafanyika mahala pa siri sana yanaendelea vizuri, kwa picha zaidi za timu hii tukutane hapahapa wiki ijayo

Comments