PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BEI YA SOSEJI TU HUYU MWANAUME ANALALAMIKA

Mdada baada ya kuolewa kwa siku chache kampigia simu mama yake;
MDADA: Mama mi ndoa imenishinda huyu mwanaume ana gubu la ajabu, ananipigia kelele hata vitu vidogo
MAMA: kwani vipi tena?
MDADA: Jana nimemtengenezea soseji 2 badala ya kushukuru kaanza kulalamika eti natumia hela hovyo
MAMA: Hapo mwanaume huna, he  mbona shida, bei ya soseji mbili tu kelele
MDADA: Sio bei ya soseji ni microwave
MAMA: Mbona sasa sikuelewi
MDADA: Nilitaka kumpashia moto zile soseji ambazo kwenye mfuko wameandika tumia microwave, ndio nikakodi taxi nikaenda supamaketi nikanunua microwave mpya , mume wangu apate soseji za moto, kurudi badala ya kuaprishieti ananipigia kelele.

Comments