PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BABA MLETE MBWA CHUONI AJIFUNZE KUSOMA

Jamaa kaingia chuo katikati ya simesta kaishiwa akamuandikia baba yake barua. 'Chuoni mambo mazuri sana, kuna maajabu hapa maprofesa hapa wamegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea, mlete BINGO na shilingi laki 5, baada ya muda atakuwa anaweza kuongea. Mzee wa watu haraka akatuma mkwanja na mbwa, haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Denti akamtumia baba yake barua nyingine kuwa wameboresha program sasa wanaweza kumfundisha BINGO kusoma, mzee aongeze kimilioni tu. Mzee wa watu aliyekuwa tayari anajisifu kijiji kizima kuhusu mbwa wake anayeongea,  akauza ng'ombe akatuma mkwanja. Likizo ikafika Denti akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake kijijini. Alipofika tu kwao  baba yake akamuulizia BINGO. Denti akamuita baba yake pembeni,' Baba hili nitakalokwambia sitaki mama asikie'. Baba akauliza,'Vipi tena?'. Denti akaanza,' Ijumaa iliyopita tumeamka vizuri na BINGO, yeye kama kawaida yake akaenda kuchukua gazeti la Ijumaa na kukaa kwenye kiti na kuanza kusoma, ghafla wakati anasoma akaniita akanambia hivi, 'Baba yako bado anaendelea na kale kachangudoa ka pale mtaa wa pili, naona hapa wameandika stori yake?', Baba kwa kweli  nilishtuka'. Baba akaingilia kati,'Ungemuua hapo hapo mbwa mshenzi huyu anataka kuniharibia mambo yangu?', Denti akajibu,'Baba na mimi lilinijia wazo hilohilo sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa'. Baba akamsifu mwanae'Safi sana safi sana mwanangu, una akili sana
'

Comments