PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

AISE POLE INSHU KAMA HII ILINIKUTA MBEYA

Mke alikuwa anajua kuwa mumewe yuko safari na hatarudi kwa wiki nzima, akamkaribisha mpenzi kwake, kwenye saa 6 usiku siku hiyohiyo mumewe akapiga hodi, mdada akamwambia mpenzi wake simama hapo pembeni jifanye sanamu mengine niachie. Jamaa akasimama kama sanamu mke akamfungulia mumewe na kumpokea mizigo na kumkaribisha ndani. Mume akamuangalia yule jamaa kisha akamuuliza mkewe,' Nini hiki?'. Mke akajibu,' Wamachinga walipita na masanamu wanauza na mimi nikanunua moja'. Mume akajibu ,'OK'. Akaenda zake na kulala hadi kwenye saa 9 usiku akaamka, akaliendea lile sanamu akaliambia,'Pole kwa mbu ndugu yangu, heri uondoke zako mie mwenzio ishu kama hii imenikuta Mbeya kwa mdada mmoja anaitwa Flora, nikapigwa na baridi siku mbili ndio nikaweza kuondoka. Haya ondoka, usiku mwema'

Comments