PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UONGOZI MOROGORO WAINGIA KATIKA MCHAKATO WA TUZO YA CHEKANAKITIME 2013

Morogoro Bus Stand Revolving Doors teh teh teh
Blog hii isiyo na chembe cha moyo, ikiwa katika pita pita zake kufanya utafiti wa washiriki wa Chekanakitime Awards 2013, imeona ni muhimu na haki uongozi ulioweza kutumia mamilioni ya shilingi kuagiza milango hii ya kuzunguka na kisha kuijengea kibanda katikati ya uwanja wa stendi ya Morogoro, kwa kweli unastahili tuzo toka kwa blog hii iliyowahi kupata tuzo ya kuwa blog isiyo na maana kabisaa. Bado eti hata huyu mhariri feki wa blog hii anajiuliza hii milango iliwekwa ya nini? Au kwa kuwa hata Ulaya kwenye stendi nako kuna milango kama hii? Pesa za kununua milango hii zilitoka wapi? Si heri wangeipa mkwanja huo blog hii ili izunguke nchi nzima kutafuta wananihii (samahani sisemi hili neno wasije wakanihoji) wengine ili wapewe nao tuzo?

Comments