PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MUANDISHI WETU MUONGOMUONGO ATULETEA PICHA YA ANACONDA AKIMKAMUA MTU UTUMBO

Kwa mara nyingine tena tumepata muandishi wa blog mwongo kuliko blog yenyewe. Mwandishi huyu ambaye kwa usalama wake tutamuita Special Reporter eti kaja na ripoti kuwa eti kamkuta Anaconda anamkamua mtu utumbo. Yaani ili kumuumbua kwa uwongo wake viongozi wasio na msimamo thabiti wa blog hii wakamdai atoe ushahidi kushuhudia huo ushuhuda wake  uliokaa kidakudaku. Kwa mshangao wa wote akatoa picha ambayo inamueonyesha Anaconda akimkamua mtu utumbo mbavu, miguu na mikono. Uchunguzi wa muda mrefu umeliacha jopo la wataalamu wetu wakiwa bado hawajaamua kama picha hii ni ya kutengeneza au ni laivu bila chenga. Sasa tunawaachia wasomaji wetu ambao hata sisi hatuwaamini watoe mtizamo wao je picha hii ni picha au foto?


Comments