HATUPIMI BANDO

17 June 2013

MSANII MAD MAVOCO AJIUNGA NA BLOG, AMETEULIWA KUWA BALOZI WA BLOG HII TATA


Blog hii ya ajabu ajabu eti imemuajiri msanii wa kizazi kipya MAD MAVOCO awe anatunga mistari, tatizo ni kuwa mabosi na wakurugenzi wa Blog wanasema huyu fala tusimstue kuwa kuna sheria ya hakimiliki wacha tu amwage mistari bure. Akitoa singo yake blog inakuwa meneja inakunja mkwanja mrefu halafu fala anapewa mfupi, au hapewi kabisa, akiulizia tunatishia kumuachisha kazi. MAD MAVOCO katoa mistari ya leo. Si unajua inshu za hapa nchini, kama unaweza kuingia mitini na mkwanja wa mtu kwa kumuuzia mbuzi kwenye gunia ruksa au vipi?
 Acha kurukaruka, acha kuchekacheka,
Wenzio wanatajirika,
We unaishia kucheka,
Chekachekacheka hahahahaha
Wenzio wanachikicha
Unanunua kila kukicha
Wanakuuzia hewa kwa bei ya mchicha,
Nuna nao mwanangu Nuna nao

No comments: