HATUPIMI BANDO

13 June 2013

MAJANGA UKWENI TENA MAJANGA MAKUBWA

Majanga tena big majanga ni pale mchumba wako uliyeamua kutulia nae anakukaribisha kukutambulisha kwa familia yake. Mimacho inakutoka kama mjusi kabanwa na mlango pale
unapokuta kumbe kaka yake alikuwa bwana wako wa zamani, dadake mmetoka kugombania bwana Maisha Hall wiki iliyopita, mama yake ni nesi aliyekubembeleza usitoe mimba siku moja ukaitoa, na baba yake ndiye baby aliye kununulia Samsung Galaxy S4 unayoitumia.

No comments: