HATUPIMI BANDO

17 June 2013

KUWA WA KWANZA KUJUA MBINU YA KIJADI ILIYOTUMIWA NA IVORY COAST KUTUFUNGA.

Baada ya kuiangalia kwa makini picha iliyotoka kwenye magazeti kadhaa wiki iliyopita ikiwaonyesha wachezaji wawili wa timu ya Ivory Coast wakiwa wametoka mishipa katika kile kilichoonekana ni kupigana, Mhariri Asiye Mkuu, Mpicha piga asiye mkuu na waandishi wote wa blog hii kwa ujumla tuliona kuna kitu siyo sawa kabisaaaaaa. Ili kuondoa utata tukaona ni vyema tukaenda kwa mtaalam. Kila Mwafrika anajua kuwa wataalamu huwa wanamajibu ya kila kitu, wakiangalia kwenye tunguli zao wanajua nini kinaendelea. Hivyo meneja utaalamu wa Blog akaenda kwa mtaalamu kuulizia kuhusu picha ile, na kwa mara ya kwanza tumepata majibu yasiyo na ubishi, ambayo yatashtua ulimwengu wa soka. 
Mtaalamu aliangalia katika TV yake ya kiasili ambayo kwetu ni ungo wa kawaida tu kumbe kwake anaona picha kama vile anaking'amuzi na kugundua kuwa wale wachezaji wawili walikuwa wana ekti kusudi mganga wao aloge ili timu yao ishinde. Ukiangalia kwa makini utakuta mganga wao hapo pichani hana nguo kabisa kavaa viatu na soksi nyeupe tu, na anajidai anawaamulia kumbe anafanya vitu vyake, umeonaee.  Kosa tulilofanya ni kuweka ile picha hadharani hivyo wote walioiona wamepatwa na madhara hayo na ndio maana tukafungwa bao nne, tena zilikuwa ziwe kumi na nane ila tu bahati nzuri kuna mtaalamu mmoja toka Kisiju alishtuka dakika ya mwisho akaanza kuweka rivas lakini ndio hivyo tena. Mtaalamu ametupa ushauri kuwa ikiwa kutakuja tena timu nyingine wachezaji wao wakapigana uwanjani, ili kutegua italazimika watanzania wote tusivuke barabara siku hiyo, na kama unatembea kivuli chako kiko kushoto, wewe pita kulia, kama kiko kulia wewe pita kushoto, hapo hata ije Man U au Man City, ni mwendo wa kuwatandika mbao tano au sita tukifuata ushauri huu. Kwa mabao zaidi kuna dawa Watanzania wote italazimika tupake usoni siku hiyo. Tunawaomba wale ambao wako na ukaribu na watu wa FAT wapeleke hii taarifa mapema kwa manufaa ya soka letu.

No comments: