PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

ETI WANAUME HAWAWEZI KUVUNJA UNGO...UWONGO MTUPU WANAWEZA

Watafiti makini wa blog hii wamegundua kuwa wanaume wengi wana nyanyaswa kijinsia halafu hawasemi. Kwa hiyo bodi ya wakurugenzi ya Blog imetoa maagizo kuwa blog hii iwe mtetezi wa wanaume ambao wananyanyaswa bila kosa lolote, na kwa kuwa tu maskini wamezaliwa wanaume, hii sio haki kabisa kikatiba. Wanaume huwa wananyanyasika halafu kwa aibu au mara nyingine baada ya kipigo kikali wananyamaza tu hawasemi kumbe wanaumia ndani kwa ndani. Blog hii ambayo imefungwa mtambo wa kurekibisha tabia leo unaanza ukombozi wa wanaume kwa sentensi ya kudhalilisha sana eti 'WANAUME HAWAWEZI KUVUNJA UNGO'. Hakuna kitu cha kudhalilisha kama hiki, na wanaume wengi hukaa kimya na kumezea tu wanaposikia sentensi hii dhalimu. Labda utaniuliza kwa nini wanaume wanakubali kudhalilishwa namna hii?  Utafiti umeonyesha kuwa wanaumbe ni viumbe wapole sana wasiopenda fujo, hivyo wakisikia neno hilo huwa hawabishi wanajinyamazia tu. Lakini je ni kweli mwanaume mwenye nguvu zako timamu huwezi kuvunja ungo? Utafiti umeonyesha wanaume wanaweza kabisa kuvunja ungo ila hawataki tu, mwanaume akiukamata vizuri ungo anaweza kuuvunja hata kwa mikono na akishindwa ataukanyagakanyaga kwa miguu lazima uvunjike. Hivyo basi wanaume wote kwa pamoja tusimame tuseme kwa pamoja  ''TUNAWEZA KUVUNJA UNGOOOOOO


Comments