HATUPIMI BANDO

21 June 2013

ETI BLOG HII NAYO YACHAMBUA SOKA (TAHITI VS SPAIN).. SPAIN YALAZIMISHA MAGOLI

Leo tumeona tumpe nafasi mchambuzi wetu wa soka atuchambulie mechi kati ya Spain na Tahiti. Karibu mtaalam Je, umeonaje mechi?
MTAALAM: Kwa kweli mechi ilikuwa kali iliyochezwa kiufundi kwa timu zote kutumia inteligent pass, ukiangalia ile dakika ya 12, Spain wakimtumia yule kiungo wao walitumia tektiko passing na kuweza kuovalep kule nyuma, kitu kilichosababisha koch wa hawa Tahiti, kufanya chenjiz kwenye lain up yake ambapo akamuingiza mtu wa kuwa anashuka na kupanda kule wing ya kushoto. Nadhani koch wa Spain alisoma ile muv ndo ukaona kamuondoa wing wa kushoto na kumrudisha nyuma ili aweze kulinda ngome.
MHARIRI: Mtaalamu labda tueleze, tuliona wakati fulani Spain wanachezea wing a kulia tu
MTAALAM: Ndio hiyo ilikuwa the kamikaze muv, ndi maana ukamuona mchezo umegein spid. Ile haf ya pili koch wa Tahiti alichenj mchezo  akawa anamruhusu kipa apande mpaka huku juu kwa winga wa kati, na ndio kosa alilofanya, tunaloweza kuliita tektiko era. Kitu ninachoshangaa kwa nini walikubali kuruhusu magoli ya chenga za maudhi, kwenye sheria za FAFI ukurasa wa tatu marufuku kufunga kwa chenga.
Lakini hawa Tahiti wakicheza na Kihesa Stars tungeweza kuona wakifunguka sana

No comments: