PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BLOG YAKO INAKULETEA CHEKANAKITIME AWARDS 2013

Chekanakitime Award
Baada ya kuangalia mambo yanavyokwenda na kusikiliza ushauri wa kutumia opotyunitii inapotokea blog hii imeona opotyunitii ya kuendesha ChekanaKitime Awards 2013.  
 Kuna kategori nyingi ambazo hazijashughulikiwa kwa hiyo wahariri na wananchi na wadau wa blog hii ya ajabuajabu, tunataka kuanza nazo, mwaka kesho tutaongeza kategori kutegemea na ushauri wa wataalamu wetu waliobobea katika mambo yasiyo na msingi. Tafadhali ukiona mtu au kundi linafaa katika kategori yoyote tuletee ujumbe kupitia blog hii. 
Sasa kwa kuwa wanamuziki walisumbua sana watu kwa kutumia simu zao kujipigia kura kwenye Tuzo zilizopita karibuni, hatutatumia mesej za simu  tutafanya mambo kivyetuvyetu. Ila ndugu wanancnhi na msio wananchi tumeni mapendekezo yenu tupate watu wa kuchukua Tuzo hizi zisizo na maana yoyote Tanzania wala mahala popote duniani:-


1.     Wimbo wa kukopi na kupesti wa mwaka………………………

2.     Wimbo usio na kichwa wala mguu wa mwaka…………………….

3.     RnB isiyo RnB ya mwaka…………………………….

4.      Wimbo wa Kinaijeria unaodaiwa Tanzania pop wa mwaka…………….

5.     Wimbo wa Kisauzafrika unaodaiwa Tanzania Pop wa mwaka…………..

6.     Wimbo usio wa kiasili unadaiwa kuwa wa kiasili wa mwaka…………………

7.     Mumbaji wa kiume aliyeimba vibaya wa mwaka………..

8.     Muimbaji wa kike aliyeimba vibaya wa mwaka………….

9.     Mwanamuziki feki wa kike wa mwaka……………………

10. Mwanamuziki feki wa kiume wa mwaka………………………..

11. Kampuni bingwa ya kutapeli wanamuziki ya mwaka………………….

12. Kinara wa kutapeli wanamuziki wa mwaka…………………………

13. Tuzo feki za mwaka……………………………………

Haya tena kivyetuvyetu tupate watu wetu wa yale mambo yetu

Comments