HATUPIMI BANDO

13 May 2013

WASHA BRENDER

Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa brender nisikie.....mke akawasha brender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha brender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa  ntarudi baada ya masaa mawili
Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na brender toka asubuhi

No comments: