PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

WABABU WAKASIRIKA WAANZA KUPATA WATOTO...CHEZEA BABU WEWE

Katika hali ambayo blog hii imegundua kuwa inayoonyesha wababu wamekasirika sana, wababu kadhaa wamewazalisha wake zao vibebi vizuuri.
Mzee Ramajit Raghav mwenye miaka 94 toka India kahakikisha mkewe Shakuntala mwenye umri wa miaka 59 kapata mimba na kuzaa kabebi wamekaita Karamjit. 
Mbabu mwingine Raymond Calvert ametambuliwa kuwa ni baba mpya mzee kuliko wote Uingereza, akiwa na mke wake Charlotte wamekazaa kabebi wamekapa jina la Jamie Rai, ni wazi wababu sasa wameona waweke moto chini ili kurudisha heshima, maana hii ishu ya kuanza kuita vibabu bebi naona ndio imeleta hii dharuba mpya ya kuzalisha kwa kwenda mbele. Tuone nani Baby sasa.
 

Comments