HATUPIMI BANDO

10 May 2013

UGONJWA WA KUTAFUNANA MIDOMO WAINGIA NCHINI

Katika hali ambayo imeiacha nchi katika taaharuki, ni huu ugonjwa mpya unaoitwa dendalyasis, ambao unaonekana kuanza kushika kasi ya ajabu. Mwezi mmoja uliopita wadada fulani walikutwa wakitafunana midomo hadharani, sasa wengine tena wamekutwa hivyohivyo. Daktari maarufu tunaemtumia kwenye blog hii Dr Pimbi amesema ugonjwa huu ambao huwaathiri zaidi wadada, ni hatari sana maana hupoteza kumbukumbu zao za namna ya kupika ugali kwa sambusa. Dalili za ugonjwa huu ni mdada kusaka midomo ya mdada mwingine kwa udi na uvumba, na kisha kuitafuna kabisa kisibaki kitu. Tunaomba silikali yenyu sikivu isisikilize kabisa kilio cha waathirika kuwa watafutiwe dawa, hakuna dawa hapo.

No comments: