HATUPIMI BANDO

19 May 2013

UCHAMBUZI WA VICHWA VYA PANZI VYA HABARI KUTOKA MANYUZPEPA YETU

 Kila siku mi nawaambia watu wasiende Uganda kula wadudu, kuleni wadudu hapahapa Bongo, mnaona sasa mmenda kule mmeharisha, hivi hamuoni kuwa mmeliletea aibu Taifa letu changa lenye timu ya mpira kubwa kama Yanga? Serikali yetu sikivu lazima ilivalie njuga hili, watu wakitaka kuharisha waharishe hapahapa nchini kwetu. Serikali itenge bajeti kwa hilo
Mharirishaji

Baada ya kuonekana limefanikiwa sana katika shughuli za utangazaji, blog hii ina wasiwasi kuwa serikali imeona iliiongezee majukumu shirika hili Tanzu lifanye kazi sambamba na lile jingine la TBS. Hii itasaidia magorofa yasianguke wala hata vibanda vya chips visianguke.  Hongera kwa ubunifu huu wa hali ya juu.

 Nchi hii watu hawaielewi tu, ina mambo mengi sana ya ubunifu wa hali ya juu. Wachina na Wahindi wamekuwa wanapata tabu sana kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa wameshindwa, sasa hapa tumepata ubunifu uliotukuka wa kuweza kuwabana wapachika mimba, yaani hapa ndipo chanzo cha mimba, ubunifu huu ukiuzwa katika nchi kama China kwa kweli nchi yetu itaingiza kipato kikubwa cha fedha za kigeni.
Mhariri wenu.

 UONGOZI WA BLOG HII, WAFANYAKAZI WAKE, NDUGU NA JAMAA NA MAADUI BADO TUNATAFAKARI HAPA KICHWA HIKI KINA MAANA GANI. TUMEGUGO YAMETOKA MAJIBU HAYA .......??????????!@#$%^&*().....KWA HIYO TAFADHALI MBUNGE WA JIMBO LETU FUATILIA HII, MAANA INAWEZEKANA NI NJAMA ZA CHAMA TAWALA

Stori inasema jamaa kaishia kufungwa miaka mitano. Sasa swali 'biskuti'hii ilikuwa ya aina gani? Au ni ile ya kizungu, watu wengine my waifu wao wanamuitaga, my sweety, my honey, my biskuti. So maybe huyu mjinga alienda kuiba my biskuti ya DC, hapo hata ingekuwa mimi, uniibie my biskuti wangu hivihivi laivu, dah lazima ufungwe bwana
By Mharishaji

No comments: