HATUPIMI BANDO

20 May 2013

UCHAMBUZI WA VICHWA VYA HABARI ZA LEO, KUTOKA KWENYE NYUZPEPA ZILIZONUNULIWA TANDALE MJINI

 Mihogo ya kukaangwa huwa mitamu sana japo jambo la kusikitisha huwa wakaanga mihogo wengine wanatumia mafuta ya ajabu sana sijui ni ya transfoma hata haieleweki, so, kwa hiyo kwa kuwa ni wiki nzima hili litaendelea wapenzi wa Mihogo watafurahi sana. Swala la pili mpaka sasa Mhariri wetu ana gugo kujua hapa pia zitakaangwa karanga au kangara, kama ni karanga gud news kwa Wanyamwezi lakini kama ni kangara najua kutakuweko na maandamano ya kupinga pombe hii maarufu kutengenezwa kwa mfumo wa kukaanga, blog hii isiyo na ukweli wowote inafuatilia hii ishu.

Kiukweli ukisikia maajabu ya dunia ni hii habari, kwa jicho la kawaida ambalo ni la kawaida, na wewe kama wewe utadhani ni jambo la kawaida lakini kwa waandishi wetu ambao wamepata vyeti vyao kutokana na kugugo kwa hiyo wana jicho la tatu, wamegundua maana halisi ya hii hedlain. Ni kwamba kuna gari la polisi lililokamatwa na bangi ukurasa wa pili. Nadhani wote mtakubaliana nami kuwa haya ni maajabu sana, hili gari lilikuwa linatafuta nini ukurasa wa pili? Nadhani Wizara husika itowe maelezo kama magari ya serikali siku hizi yanaruhusiwa kurandaranda kwenye kurasa za magazeti.

Sasa jamani tuwe wa kweli, wakati umefika kujiuliza tunaenda wapi, wakati tunataarifiwa kuwa JK (John Kitime?) atakuwa akishuhudia Mawaziri watatu wakivuana nguo. Blog hii imemtuma mpicha piga wetu maarufu ahakikishe anarudi na picha za tukio, maana hii itaweza kupandisha chati ya blog hii isiyo na maana kiasi cha wale Mamaketing Meneja wanaosomaga blog hii kila siku kwa makini kuliko vitabu vya dini zao, pepo wa kunyima tangazo blog hii awatoke na ashindwe katika jina la JK(John Kitime). Ene weyi tatizo ni bado tunapeleleza wapi tukio hili la kihistoria linafanika, tumejaribu mpaka kugugo kichina hatujapata jibu. Lakini tunawahakikishia wasomaji wetu wapendwa ambao mnaweza kudanganyika kuwa tutaendelea kuwaletea ripoti kuhusu ishu hii ya kuvuana nguo.

No comments: