HATUPIMI BANDO

3 May 2013

UCHAMBUZI WA VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YETU

 Kwa kweli kichwa hiki cha habari kitatikisa ulimwengu. Unakumbuka kuwa Loliondo ndiko kulikuwa na ule muujiza mkali wa Babu kuwapa watu kikombe na wakapona magonjwa mengi ya ajabu, sasa maajabu haya mapya ni kiboko. Bado blog yako isiyo na chochote cha maana inafanya upelelezi huyu Waziri alifanya nini mpaka akageuka au akageuzwa Mbogo. Kwa wale wa kuja Mbogo ni jina jingine kwa mnyama aitwae Nyati. Kiukweli kama kuna mtu huko ambaye ametumia uchawi wa kumgeuza Waziri Nyati ni muhimu serikali imtafute ili aweze kutumiwa kwa matumizi ya kufwata sheria bila shuruti, na kugeuza watu wakorofi wawe panya au sisimizi na kadhalika. Kwa sasa tunatoa tahadhari kwa wanaokwenda Loliondo wajichunge sana miujiza huko ni mikubwa sana.

 Kama blog inayohusiana kwa karibu kabisa na jamii, tumeshtushwa kuwa kuna wanga wengine wanajipa sifa kuwa wao ni wanga wa jamii, je, ni kitu gani cha ki uwanga uwanga kilichofanywa mpaka mtu akajipa sifa kuwa yeye ni mwanga wa jamii? Je, kulikuwa na BSS ya kushindanisha wanga na yeye akashinda? Blog yenu imekwisha tuma jopo la wanga waende kumtesti huyu mwanga na kuona kama kweli anastahili sifa ya kuitwa mwanga wa jamii yetu.

Hakuna kitu kinauma kama kushikwa pabaya hasa ukiwa mwanaume, na swali, ni kwanini watu washikane pabaya? Tena kwenye TV 'live'?, maana blog hii imegundua kuwa kila kinachoendelea Bungeni kinaonyeshwa live kwenye luninga, sasa hii ishu ya wakubwa wazima kushikana pabaya inalaaniwa na blog hii

No comments: