PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UCHAGUZI 2015, WENYE BLOG KUWA NA UWAKILISHI BUNGENI

Katika kile kinachoonyesha kukua kwa domokrasia, waandishi wa blog watakuwa na muwakilishi wao Bunge lijalo. Hii itakuwa inawapa wananchi habari live bila chenga kutoka mjengoni. Mpaka sasa haijaamuliwa kuwa uwakilishi huu utatokana na vyama vya siasa au wananchi hawa wataanzisha chama chao cha siasa cha kutetea mstakabali wa teknolojia ya dijitali au la. Kimsingi blog hii imeshateuliwa kuwa ndio Mbunge wa kwanza wa Mablog , kwa wale ambao watakataa itaonyesha dhahiri kuwa demokrasia imekomaa maana ubishi kwenye demoklasia ndio kigezo cha mafanikio. Na inawezekana blog hii ikachaguliwa kuwa Waziri Mkuu, hapo ndipo utamu utakolea. TOA MAONI YAKO KUPITIA BLOG HII< UKIPINGA TU UJUE WEWE NI MPINZANI

Comments