HATUPIMI BANDO

20 May 2013

SHKAMOO MWENYE PICHA HII

Uongozi uliotukuka, bodi ya wakurugenzi, wafanyakazi, vidampa, ndugu, jamaa, maadui, marafiki, wapambe, wanafiki na kadhalika wa blog hii wameona watumie asubuhi hii kusema 'Shkamoo kwa yoyote mwenye picha hii' Katika kikao cha wafanyakazi wa blog hii kilichofanyika huko Iringa vijijini baada ya kukimbizwa na mabom pale Iringa mjini, wote tulikubaliana kumpa shkamoo huyu  mwenye picha japo katibu wa kikao alisahau kuandika jina la mwenye picha na sababu ya uamuzi huu wenye kutukuka, hivyo maamuzi yalisomeka hivi,
 1. Katika kikao hiki kilichokuwa hakina mwenyekiti, wala mwenye meza, wala hata mwenye deski, wajumbe kwa kauli moja wamesema Shkamoo mwenye picha
Na hivyo basi blog kwa kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya kikao tunasisitiza kuwa tunasema shkamoo mwenye picha.

3 comments:

Cathbert Kajuna said...

Shikamoooo brazaaaaaa

MUHIDIN MICHUZI said...

MARHABAAAAAAAAAAAAAA.....

John Kitime said...

Asante mzee, hawa watoto wakina Cathbert ngoja waone sura yako wakati uko umri wao