HATUPIMI BANDO

13 May 2013

MHARIRI WA BLOG HII AFUKUZWA KAZI KWA KUSABABISHA BREAKING NEWS

Wakurugenzi wa blog hii baada ya kurudi zao maskani wakitokea sehemu kama Coco Beach, Msichoke Club na sehemu za ajabu ajabu kama hizo, walishikwa na butwaa baada ya kukuta Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Usanifu na Hadidu Rejea Kuu Za Blog, kaweka picha hizi mbili kwenye blog. Hivyo ikalazimika kikao cha bodi ya blog kukaa chini kwenye mkeka na kuamua kumfukuza kazi bila kumlipa mshahara wala NSSF, NPF, CUF na wala kumrudishia returns za Income Tax, wala kumlipa kiinua tumbo, mhariri huyu kwa kuwa kasababisha blog iwe na Breaking Nyuz kitu ambacho blog hii haitaki kabisa na ni kinyume cha Mipango Mikakati ya blog hii. Pia uongozi wa blog umeazimia kuhakikisha unaeneza majungu ili mtu huyu asiajiriwe katika chombo chochote cha habari ambacho hakina maana yoyote nchini na angani.


1 comment:

Focus Mushi said...

duuh noumar kweli mzee wangu