HATUPIMI BANDO

22 May 2013

MAGAZETINI LEO UTATA UNAENDELEA ....Mwakyembe na ishu ya ndege, CCM yanawa, Lema mwanamichezo!!!!!

 YAANI weee acha tu. Mbona hakuna siri, mbona jambo liko wazi kabisa. Hebu fikiria  kidogo tu, pamoja na mshahara na marupurupu yake yooote ya Uwaziri na pia angeongezea na michango ya wananchi wa jimbo lake kwa mtazamo wangu ni kuwa mkwanja wa kununulia ndege ungekuwa bado kukamilika, au hela ya kupeleka ndege sevis ingekataa tu.  Alafu kuna ishu nyingine ya ziada,  akishanunua ndege si atakuwa anatua Mbeya pale Mafiati, halafu analazimika kupanda Vimzunguko kwenda jimboni kwake so why anunue ndege? Eh why?

 Bodi ya wahariri wa blog hii hawajakielewa sawasawa kichwa hiki cha mwendawa....sori cha habari toka gazeti moja maarufuku, kimekaa kiupande upande, huyu Lema alikuwa anachezea matope? Au yaani what is this? Ngoja tugugo, please subirini hapohapo msiondoke
 
Kuna kunawa mikono kabla ya kula, na kunawa mikono baada ya kula, wachunguzi wetu toka shirika la Kimarikani la FIB wako kazini  kuchunguza nini kitatokea au kilishatokea......... Hii tutaipata laivu no googling

No comments: