HATUPIMI BANDO

20 May 2013

JE MPICHA PIGA WETU MUONGO? UMMA TUSAIDIENI

Mpicha piga mkuu wa hii blog (jina tunalihifadhi kwa usalama wake) amedai alipiga picha hii uwanja wa Taifa juzi kabla tu ya mechi ile ya watani wa Jadi. Kwa vile blog hii saa nyingine ni ya kiheshima kutokana na Mbunge mashuhuri kusema huwa anaisoma na ina mpa pointi za kuzungumza mjengoni, tumeona tuandae tume ambayo itategemea kupata fungu la fedha za kukamilishia kazi hii muhimu kitaifa toka Wizara ambayo makadirio yake yamekwama baada ya kuingiliwa na sugu, ili kuweza kukamilisha uchunguzi wa uwongo au ukweli wa madai haya.  Tume hii ya watu sita itakuwa chini ya blogger maarufu Henry Mdimu (kama akikubali), itatakiwa kwanza iandae hadidu rejea zake, kisha kupanga mpango mkakati wa jinsi gani wataliangalia hili swala, kisha kuhoji japo robo tu ya watazamaji waliohudhuria mechi ile, kisha kushirikiana na vyombo vya dola kutumia utaalamu wake kuona kama kweli piga ilipichwa juzi. Pichani ni Mzee Mengi, Mzee Adam Dewji na kakijana ambako kama wahariri hatukuweza kukatambua japo mpiga anadai eti ni mwenyekiti wa klabu. Ene wei kamati itasimamiwa na mimi mwenyewe JK(John Kitime) baada ya kuombwa na mamia ya Watanzania wakiwemo polisi shirikishi wa Kwa Mtogole. Aksanteni kwa kunisikiliza.

No comments: