HATUPIMI BANDO

3 May 2013

HAKUNA BREAKING NEWSSSSS HAPA -BARCELONA KUBADILI JINA NA KUITWA SEVEN UP

Kumbe kile kitendo cha Barcelona kuachia mbao saba bila kujitetea, kilikuwa ni mpango wa kibiashara ili kupata udhamini wa soda maarufu ya 7up. Mfanya kazi mmoja wa kampuni ya soda hii ambaye alikutana na muandishi wetu katika baa moja pale Sinza Mapambano, aliitoa siri hii baada ya wote wawili kuwa njwii kwa viroba vya  Konyagi iliyopozwa na 7up, na pia kutoa siri kuwa inawezekana kocha Morinyo akaja pale Mwenge kiwandani ili kuja kuchukua jezi za timu. Inasemekana press conference ya jambo hili kubwa itafanyika katika bar moja huko Tandika.

No comments: