PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BREAKING NEWSSSSS(kwa mara ya kwanza) BLOGGER MAARUFU APATA MTOTO MPYAA WA KIUME, mtoto azaliwa na kipaji cha kublog

Yule blogger wa http://kajunason.blogspot.com/ bwana Cuthbert Kajuna, leo kadhihirisha kuwa ni mjanja fulani baada ya mkewe mpendwa kujifungua mtoto wa kiume ambaye mara baada ya kutoka hospitali alionyesha kila dalili za kuwa blogger kutokana na kitendo chake cha kulilia maus ya laptop ya baba yake. Blogger wengine kama yule wa ile blog ya othmanmichuzi.blogspot.com/ 
walionyeshwa kushangazwa sana na tukio hilo, ila yule mzee wa busara wa  mdimuz.blogspot.com/  aliwakumbusha kuwa alipokuwa mdogo alisikia wazee wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka, hivyo basi mtoto wa blogger ni blo ni blogger. Blog hii isiyo na maana kabisa ilijaribu kuwasiliana na mama wa mtoto simu yake ikawa inaitaa tu, wapicha piga wetu walipotumwa kumpicha piga huyu blogger mpya wakarudi na picha hii hapa. Mpaka sasa mhariri bado haamini kuwa hii ni damu ya Kajuna, hivyo ukweli kuhusu picha hii unaendelea kutafutwa.
Blog hii isiyo na maana inampa hongera huyu mzee na mkewe kwa kupata mtoto MPYA KABISAAAAAAA

Comments