HATUPIMI BANDO

22 May 2013

BLOG YA CHEKANAKITIME KUANZISHA MASHINDANO YA BLOGGERS 2013....JANDIKISHE

Kutoka na maendeleo makubwa sana ya Blogging hapa Tanzania, blog hii isiyo na maana wala breaking news wala nini, tena hata sijui kwanini watu wanaisoma, imeamua kuanzisha mashindano ya Blogs. 
Kamati ya mashindano haya iliyofanya mkutano wake mkuu pale Pikolo hotel jana na kutumia maelfu ya fedha kwa chakula tu, iliamua kuna umuhimu wa kufanya mashindano haya ambayo yataweza kuendeleza fani hii ya blogging.
Ndugu wananchi napenda kwa maneno haya machache kuzindua mpambano wa mkali wa  BLOG BINGWA YA KUCOPY NA KUPASTE 2013
Taaluma hii ambayo inakuja juu sana ni muhimu itafutiwe zawadi, katika kipindi kifupi kijacho tutatangaza wadhamini, najua hii haitakuwa tatizo, kwa sababu na wadhamini wengi ni mabingwa wa kukopi na kupesti hivyo watajitokeza tu. Tafadhali orodhesha jina la blog yako hapa ili uweze kuwemo katika mchakato wa mashindano. Tunajua kuna wale mabingwa wanaweza kushindwa kujiandikisha kwa sababu mbili au tatu, tutawaandikisha kwa nguvu za dola. Karibuni sana Makoooooofiiiiiiiiiiiiiiiii pwa pwa pwa pwa pwa

No comments: