HATUPIMI BANDO

9 May 2013

BABA MI NIMETOKA WAPI?


DOGO: Baba kwani mimi nimetoka wapi?
BABA: Dah mwanangu mbona unaniuliza swali gumu hivyo? Ene wei hebu kaa hapo nikuhadithie. Mimi nilikutana na mama yako siku moja wakati anatoka kazini, tulikutana kituo cha basi, mvua kubwa ikaanza ikalazimika tuchelewe sana kupanda basi, hivyo tukazoeana sana. Baada ya kama miezi mitatu tukaona ni vema tuoane, tukawaeleza wazazi wetu wakatukubali, harusi ikafanyika, tena kubwa sana, tukaanza kuishi pamoja na kwa kifupi ndio wewe ukapatikana. Ukikua kidogo utanielewa nina maana gani
DOGO: Haya, ila mwalimu atanipiga nisipomwambia kesho, katuambia wote tuwaulize wazazi wetu tumetoka wapi. Mwalimu wetu kasema yeye ametoka Bukoba

1 comment:

Anonymous said...

Hahahaha! Baba kawaza tofauti.