PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

WATANZANIA TUMEKUWA WA 6 KWA KUKATAA POMBE ZA KUZUNGU
Utafiti wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kukataa kunywa pombe za kigeni (mawhisky, mabrandy, mabia na uchafu mwingine).

Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe walioipenda ijulikanayo  kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.

Kwa mujibu wa utafiti huo,Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52,ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07. Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa za asili.

Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.

Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa , eti  aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo zenye historia ndefu kwa sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama kwa wazungu.

Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya za wageni watakaoonja pombe hizo.“Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini,moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza, lakini hakusema kuwa jambo  hili pia linatokea kwa pombe za kizungu.

Dk  pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo, inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” Japo wote tunajua kuwa kusahau ni aina ya kupunguza mawazo.
Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya. Kwa mfano kama huna ada ya shule kwa wanao nenda kituo cha afya upate ushauri nasaha, utaondoa msongo.
 
Katika miaka ya hivi karibuni,kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine. Hapa tunazungumzia pombe za kiafrika tu za kizungu kunyweni ni safi zana kwa kuondoa msongo wa mawazo.

Comments

nyandaro said…
since its a made in tanzania it is grate its better to kill ur self than being killed wadhungu's liquor got chemical but our from natural raw materials ryt guys?MADE IN TANZANIA………!
nyandaro said…
nadhani hii inadhihirisha ni jinsi gani hatuko nyuma katika kujiajiri na kupenda bidhaa za nchini kwetu madaktari wanajua kwamba pombe ni pombe mazingira ni kigezo tu kwahivyo hakuna tofauti kati ya wisky scoatch konyagi na gongo ingawa vyote vinalevya vinatengenezwa mahali tofauti hvyo mazingira ni kigezo kinachogombwa ni kwamc watanzania tunywe kwa afya au starehe tena kwakipimo maalum kisichozidi tukizingatia kwamba unywajipombe kupita kiasi ni hatari kwa afya zetu,nawapenda sana