PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

UNAFIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII


TOFAUTI YA WADADA WENGINE NA WAKAKA WENGINE.
 MDADA 1: Hello mpenzi mambo
MDADA 2: Niko poa sweety, dah umenikumbuka mamii
MDADA 1: Yaani nimekumiss, nikaona nikupigie nikwambie leo naja kwako
MDADA 2: Dah nitafurahi kitu, jamaa shosti navunja safari zote nakusubiri
MDADA 1: Baadae sweety. Akikata simu tu  MDADA 2, anamwambia mdogo wake
MDADA 2: Yule Malaya kafosi kuja kunitembelea sijui ana umbeya gani? Au kaishiwa anataka nijee nimnunulie bia za bure, ataula wa chuya halooooo

MKAKA 1: We mwendawazimu uko wapi?
MKAKA 2: Hii kali masikini umepiga? Mkeo kakuruhusu leo ?
MKAKA 1: Hivi kwanini hujafa watu tule pilau?
MKAKA 2: Kufa sifi na leo nakuja kunywa bia bili yako, haya nikukute wapi?
MKAKA 1: Pale kwenye baa anayonywea baba yako, usipokuja ntashukuru maana hela yangu itanitosha vizuri sana. Akikata simu tu MKAKA 1 anamwambia mkewe, yaani huyu jamaa, ni rafiki yangu toka utoto, tukikutana huwa raha sana

Comments