PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

STAILI ZA KUKOPA

Jamaa zetu wale utasikia 'Hi, could you borrow me $100, will pay you back on Monday' Sasa sikiliza Mswahili.
MSWAHILI: Kaka vipi? Shwari? Dah hatuonani mzee? Vipi mishe? Mnatunyima nini? Nimekuona kwa mbali shavu dodo full kipupwe, sie tupo bwana, ila shida tu bwana, na misiba imefululiza, wife nae kajifungua ghafla, sasa kuna cheki naisubiri haijatoka mpaka leo, wanasema itatoka wiki ijayo, eti system iko daun, hapa nimekwama kidogo kama una laki moja karibu nirushie nitakurudishia mwisho wa mwezi.

Comments