PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BLOGGERS FC YAFANYA MAAJABU MZEE WA TIMU AKESHA KWENYE PIPA LA KOMONI

Leo ilikuwa siku kubwa sana kwa wana media mbalimbali hapa Dar es Salaam, kwani katika viwanja vya Leaders mamia ya wanamedia na wadogo zao, watoto wao, ndugu zao, na jirani zao walikusanyika katika viwanja hivi na kukawa na mashindano ya michezo mbalimbali. Katika mashindano hayo mchezo uliovutia kuliko yote ni ule wa soka kati ya Bloggers FC na timu iliyokusanywa harakaharaka ya Radio Maria FC. Bloggers FC ni timu ngeni kabisa katika ulimwengu wa soka lakini ilikuwa na wachezaji wenye kufanana kwa mambo mengi na wachezaji kutoka timu za Divishen ya kwanza Italia, Spain, Uingereza na Brazil, kifupi timu hii ilikuwa na majembe kama sio sululu kabisa. Timu hii ambayo ilifanya mazoezi makali kwa dakika chache kabla tu ya kuanza kwa mechi, ilifungwa kwa taabu saana katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi, kwa magoli matatu bila na timu ndogo ya Radio Maria.
Miguu ya wachezaji:
Zifuatazo ni picha miguu ya majembe hayo, katika hii picha ya kwanza  ni miguu hii hakuna shaka  ni kama Rooney ila sema ya hii  mieusi kidogo, nadhani huyu ni www.othmanmichuzi.blogspot.comKatika raundi ya kwanza timu moja pinzani (jina linahifadhiwa kwa leo), baada ya kuona aina ya miguu ya wachezaji wa Bloggers FC, ilikataa katakata kuingia uwanjani na hivyo kuipa ushindi timu hii tishio. Mtaalamu mkazi au tuseme Mzee wa kamati ya ufundi ya timu  alilazimika kwenda Iringa Vijijini kuchukua zana za kazi kuhakikisha ushindi, huyu si mwingine ila ni blogger maarufu wa Blog isiyo na maana yoyote duniani ijulikanayo kama www.chekanakitime.blogspot.com ,maarufu kwa jina la ajabu Mzee Kitime.
Mzee huyu ambaye alilazimika  kukesha kwenye pipa la pombe maarufu iitwayo komoni hii ni kusaidia timu pinzani zijisikie zimelewa komoni wakati zikiwa zinacheza na Bloggers FC, bahati mbaya alikosea masharti na kunywa soda kabla ya mechi jambo lililofanya timu yake ndio ikalewa na kujikuta imefungwa 3-0 na Radio Maria FC. Lakini baada ya kukimbia  na kufanya kafala fulani chini ya Mbuyu ulioko Kenyatta Drive mambo yalikubali na Bloggers FC wakaitandika timu ya DSJ 3-2 na kuingia fainali. Katika hali ambayo ilimshangaza hata mtaalamu aliyekuwa akimsaidia Mganga wa timu, eti ushindi ikapewa timu ya Mwana nchi FC, ushindi wa pili ikapewa Radio Maria FC na Bloggers FC eti ya tatu. Any way shukrani kubwa kwa wadhamini wa Bloggers FC  SAPPHIRE COURT HOTEL ya Jijini Dar


Comments