HATUPIMI BANDO

28 April 2013

HII SIYO BREAKING NEEEWWWWSSSSS.... hata usiposoma powa tu...MTOTO UMLEAVYO

Yaani imekuwa kawaida wamama wengine huwa wanafurahia watoto wao wadogo kutamka matusi machafu, eti ni ujanja, pambafu zenu....

BREAKING NYEUSIIIIII...PICHA YA MAZOEZI YA SIRI YA ARSENAL YAVUJA..HII HAPA

Kuna watu wengi sana wasiotaka kuamini kuwa sisi ndio namba one kwa kufichua mambo yaliyojificha katika jamii. Baada ya kumfichua Messi akiwa kajificha kule Doma Mikumi, sasa tumeweza kugundua kambi ya mazoezi ya siri ya timu maarufu duniani Asnali. Timu hii baada ya kugundua kuwa ina mchezo mgumu na Mashetaji imelazimika kujificha huko Turiani Morogoro na kufanya mazoezi makali na pia kamati za ufundi kukutana na waganga mbalimbali ambao waliihakikishia timu hii ya kutoka uwanja wa Emiret kuwa wataifunga Man U kama kile kipigo cha Wajerumani cha dozi ya fo by fo. Tumeona ili kuondoa ubishi tuweke picha hii laiv, maana wale manazi wa timu hii bingwa ya kukosa vikombe wangebisha kuwa timu yao haikuwa kwa mganga Turiani.
Mwandikaji wenu.

MESSI AKUTWA KAJIFICHA KATIKATI YA MIKUMI....Bayern wahusika

Blog yenu isiyo na habari za maana imetumia maspy wake kujaribu kumtafuta mchezaji maarufu wa Barcelona ambaye toka mechi na Bayern Munich ilivyoisha alikuwa hajulikani aliko. Baada ya msako wenye utafiti wa kutumia vyombo vya kidijitali imemgundua kajificha Mikumi. Pamoja na matatizo makubwa ya lugha maspy wetu walijaribu kumhoji kwanini kakimbilia Mikumi, kwa kiswahili kibovu sana Messi alisema,'Bayen iko ondoka? Bayen iko natisha kuliko simba ya Mikumi'. Kitu kilichodhihirika wazi maana Messi alikuwa radhi kujificha Mikumi zaidi ya wiki akiwa katikati ya simba na tembo kuliko kuwaona tena wale jamaa wa Bayern Munich. Utawala wa blog hii ambao ni mimi, ukishirikiana na staff nzima ya blog hii ambayo ni mimi tunajaribu kuwasiliana na ubalozi wa Spain ili kumkamata huyu jamaa na kumrudisha kwao. Habari zaidi zitarushwa na CNN na kadhalika tutakapowapa video nzima tuliyo nao.
Nikiripoti toka katikati ya Mikumi ni mimi Mwandiko wako

KALALE HUKOHUKO ULIKOKUWA

Waif kaenda kikao cha harusi, pombe zikamnogea kuja kushtuka ishakuwa saa sita usiku. Akarudi kwake kichwani anawaza ataingiaje kwake?  Akapata njia...................
MKE: Hodi mume wangu
MUME: Unaniona mie Bushoke sana, sifungui, rudi huko ulikokuwa kalale huko huko
MKE: Mie sikuwa nimekuja kulala, nilikuja kuchukua kondom ziko kwenye pochi yangu juu ya kabati, kuna wanaume kibao nimewaacha kule, lazima mtu uwe na kondom nyingi
MUME: Pumbavu mlevi mkubwa, ingia ndani huendi popote shenzi

HUYU BABU SI YULE WA PALE NANIHII HUYU?

Pamoja na kuwa hii ni katuni tu, huyu babu anafanana na babu moja maarufu kwa totoz au siyo. Mi sijasema mumtaje hayawahusu

WAZAZI WANGU WAPENDWA NIMEPATA MCHUMBA MZUNGU

Wazazi wapendwa ningependa kuwataarifu nimepata mchumba mzungu. Hili najua mtafurahia maana ntakuwa mtu wa kwanza katika ukoo wetu kuoa mzungu. Tena baba mzungu huyu mweupe kuliko yule padri wa pale kijijini kwetu, nawatumia picha yake. Ni msichana mwenye adabu ya kiafrika najua mama utafurahi sana 
Ni mimi mwanenu mpendwa
Mkwe wenu My sweet Dolores from Texas

HAWA WAZARAMO UKISHINDANA NAO MDOMO HUWAWEZI DAWA YAO MOJA TU HAKUNA KUONGEA


27 April 2013

YAANI SABABU ZENYEWE HAZINA SABABU KABISAAAAA


Ndugu wananchi wa hii blog isiyo na maana yoyote  hasa nchi kama China , Japan na Tibet. Leo majira ya alfajiri mpiganaji wetu mmoja kakumbwa na zahama ya kukamatwa na askari wa jiji kutokana sababu ambazo hazina sababu kabisa. Eti we fikiria aliwa kaitwa na jamaa waliokuwa wamekasirika kwa kuwa wameudhiwa, wakamuomba aje ili awaonyeshe njia ya kwenda kituo cha kumaliziza hasira wakamalize hasira zao zote unaonaee, sasa  akaona atumie busara zake ili wakasirike zaidi ili wasiwe na woga wakati wa kumalizia hasira zao. Basi akawaambia kuwa wasikubali ufala, kwanza mwenyekiti wa serikali ya mtaa wala hawajali wala nini? Kwa kuwa anagekuwa anawajali na yeye angekuja kukasirika nao  mara moja, badala yake ameonekana kuleee mitaa ya Maharage Limited Company anachekacheka kama yuko kwenye pati ya hepi bathdei tu yuu. Kumbe alikuwa anatafuta kura zilizopotea.
Kwa hiyo mwakilishi huyu wa hii blog  akawaambia jamaa "Namimi naenda chukua rungu langu tusindikizane mkaondoe hasira kwa kuwa ni haki yenu ya toka shule ya chekechekea na kwa maadili ya Kiyunani kwa kutumia lugha ya Kilatini, lazima aliyekasirika alindwe mpaka hasira zake ziishe na mtu anayembishia au kumuia asikasirike ni wazi aanaingilia haki za kipraimari za kukasirika".
Sasa jamani eti mtu kuhamasisha kidogo tu hivyo ndio wamemtait muwakilishi wa blog, eti leo hakuna ruksa kulala nyumbani, sasa nani atatuletea vichekesho wiki ijayo?
Halafu si hivyo tu kwa kupitia  mtandao wa kijamii wa twitter eti wametishia kuwa watamuwekea bangi mfukoni ili kumbambika kesi ya mauaji, yaani hiyo twitter hata Obama kaiona laiv kabisa. Bado na sisi tunaitafuta tutawaletea hapa muione laiv. Yaani inasikitisha kweli, yaani hivi kweli mtu kuhamasisha watu watumie haki yao kukasirika ni kosa kweli jamani?

25 April 2013

SIMBA MLA WATU

Jamaa aliwahi kutembelea kijiji kimoja akakuta tabia ya kule ni wanaume kutangulia mbele sana wakiwa na wake zao, ambao kama kawaida huwa wamebeba mizigo mikubwa. Baada ya miaka michache akarudi tena kwenye kijiji hicho akakuta tabia zimebadilika kabisa, wanaume walikuwa wakiwatanguliza mbele sana wake zao. Jamaa akauliza kulikoni tabia hii mpya? Akaambiwa kuna simba mla watu

24 April 2013

JE UNAJUA KUWA LEWANDOWSKI ANATOKA IRINGA VIJIJINI?


Blog yenu isiyo na jambo lolote la maana imefanya utafiti a harakaharaka na kugundua kuwa jina LEWANDOWSKY limetoka sehemu za Tanangozi pale Iringa, katika jimbo la uchaguzi la Kalenga. Siku moja mkazi mmoja wa huko aligundua mtu ameanguka huku kazungukwa na chupa nne za bia na kidumu cha Ulanzi, alipomuuliza, “We kwanini umelala hapa?” Jamaa alimjibu kilevi. “Ndo nimelewa wisky”. Mlevi huyo alipopata mtoto wa kwanza, jamaa aliyemkuta kaanguka akaamua kumuita mtoto huyo Lewa Mwa Wiski, kijana huyu akahamia Ujerumani na kuunganisha majina yake kuwa Lewandowsky,kuna tetesi kuwa kijana huyo ni mcheza soka hatari anawalewesha makipa kwa chenga zake za maudhi

21 April 2013

SEMINA KWA NDUGU ZANGU WANAOINGIA MJINI KWA MARA YA KWANZA


Je, wewe ndio unaingia mjini? Kwa kweli naona nichukue muda huu kutoa semina fupi kwako kuhusu mambo ya MUJINI. Kimsingi sentensi isemayo  'Mjini shule' ni ya kweli kabisa na ni muhimu kuiweka kichwani mara tu utakapoingia  mjini, kwa taarifa mjini ni kuanzia Chalinze. Ok kwa leo tutaanza na sentensi ambazo asilimia 99.99 ni uwongo, na utazisikia sana. Hivyo kaa chonjo
1.     ‘Kiukweli siko peke yangu, boifrend wangu yuko nje ya nchi anasoma’……hii ni sentensi ya kukufanya usimuulize inakuwaje ana maisha mazuri wakati hana kazi na na anaishi peke yake? Hapa na wewe utageuka kitega uchumi kingine, mjini utaitwa BUZI au ATM au SERIKALI na kadhalika.
2.     ‘Sijichubui ni kwa sababu ya maji ya Dar es Salaam yananirudishia rangi yangu ya asili’…..hahahahahahaha hapa na cheka tu utakuwa fala kuamini mke uliemuoa mweusi anabadilika rangi kwa ajili ya maji ya bomba, ila wako wenzio wengi wanaamini rungu hili
3.     ‘Nilienda Arusha kuna kakake rafiki yangu kanikopesha milioni 3 za kuanzia biashara. Lakini hakuni dai chochote’………….jiulize wewe huyo mdada ungeweza kumpa milioni 3 halafu kisitokee chochote?
4.     ‘Sikupendi kwa ajili ya hela yako, I love you for who you are’…….Hii sentensi hutumika sana pia na wanasiasa ambao hudai hawataki ubunge kwa ajili ya kipato bali wanataka kusaidia wananchi teh teh teh chezea Bunge wewe
5.     ‘Yule ni rafiki yangu wa kawaida tu’………hakuna kitu kama hicho hapa mjini
6.      I love u too!, Ukisikia sentensi hii ina maana umeanza wewe kwa kusema I love you, na hii ni hatari kwani ina maana umeshapoteza uwezo wako wa kuwaza sawasawa. Akili imeshasiz

CHEZEA MZUKA WEWE


KESI KUBWA MTAANI KWETU

Ndugu yetu ambaye ni msemaji mzuri sana kwenye mitandao ya kijamii aka Mbulula ana kesi mtaani kwetu. Ili kutokuingilia uhuru wa mahakama sisemi kitu tunangojea hukumu ya mahakama ambayo itampa adhabu stahili mhalifu huyu aka Mbulula. Tena ni heri mahakama ifanye kitu cha uhakika maana wananchi wenye hasira kali wanamsubiri nje ya mahakama

AJENDA ZA KIKAO CHA BANGI WIKI IJAYO, WAKILI KUTETEA WAKALA

-->
Katika kikao chetu cha bangi wiki hii, kama kawaida tutazungumzia mambo yetu ya Kibangibangi. Moja ya  ajenda itakuwa kujaribu kutafakari kwanini kampuni ya Kimataifa ya huduma za kusambaza umbeya imeamua kuuza vocha za kusuguliwa  zilizoexpaya. Na kuwaletea usumbufu mkubwa mawakala wake, jambo ambalo litasababisha kampuni kutumia mawakili kutetea mawakala. Pia katika kikao cha bangi cha wiki lijalo italazimika tuzungumzie tatizo la hizi mvua ambazo zinanyehsa bila mpango, kiasi cha watu kuonekana waongo, eti mvua inanyesha Kijitonyama wakati Sinza kukavu, au inanyesha Kariakoo wakati Ilala kukavu, serikali lazima iingilie kati ili kuwe na mpangilio unaoeleweka, mvua zimekuwa hazina mpangilio utadhani waendesha Bodaboda, hii haiwezekani, mimi kama Mbangibangi mkuu wa eneo langu ambalo wakazi wake wanaathirika kisaikolojia na hizi mvua, sasa sitaki tena kuongea na punda nataka kuongea na mwenye punda.

Pitia vichekesho nilivyotumiwa

VICHEKESHO

MKONG'OTO WA KIFUTIO


Haya wote waliowahi kuonja adhabu hii wakoment humu ndani na kueleza utamu wake

18 April 2013

KIKAO CHETU CHA BANGI KIMEAHIRISHWA MPAKA KESHO


Katika kikao chetu cha Bangi cha wiki hii tumeweza kuzungumza mengi sana yasiyo muhimu. Ni kweli tumejikusanya hapa kuwakilisha wavuta bangi wenzetu, lakini tulipofika hapa tumekuta wawakilishi wengine kumbe hata bangi hawavuti, tumejaribu kuomba muongozo kutokana na kifungu cha 6 cha makubaliano yetu kuwa …Mtu yoyote asiye vuta bangi hawezi kuwakilisha wanaovuta, na kwa hali ya ajabu sana mheshimiwa Hedfon si kaanza upendeleo, eti anajifanya stim ilimzidi hivyo hakusikia hoja hiyo, si ndio ikalazimika pale, mshika kiboko wetu akaanza kuimba mistari aliyotunga palepale akitumia sauti ya wimbo wa Azonto. Akaanza kuimba ….
Mwongozo, mwongozo, mwongozo,
tunataka mwongozo mwongozo mwongozo,
tunataka mwongozo mwongozo mwongozo…….
akaimba mpaka mheshimiwa hedfon kakasirika akaamua kusokota rizla mbili mfululizo kwa kisirani. Enewei kuna mambo yasiyo ya msingi ambayo tumekubaliana, tunataka serikali yetu itueleze kwanini inauza rizla lakini inakataza bangi? Sasa hizo rizla za nini? Pili tunataka kujua kwanini wadada wa kanga moja wamepigwa marufuku lakini wadada wenye vibikini wanaruhusiwa kwenye TV masaa 24? KIKAO CHETU KIMEAHIRISHWA MPAKA KESHO

17 April 2013

BREAKING NYEUSIIIIIIIIIIIII..BLOG INAHAMIA DODOMA

BAADA YA KUGUNDUA KUWA KUMBE CHANZO CHA KOMEDI DUNIANI KIMEHAMIA DODOMA, BLOG YENU MAARUFU KWA MAMBO YASIYO YA MAANA IMEONA ISILAZE DAMU NAYO INAHAMIA DODOMA, 

BREAKINGGGGGG NYEUSSIIIIIIIIIII...FUCK YOU YAINGIA RASMI NDANI YA MJENGO

Mbunge wetu leo  kasahau kuzima maik yake, (au alifanya makusudi), na kutamka laiv bila chenga maneno 'Fuck you' ndani ya mjengo wetu (uliokuwa) wa Heshma. Blog yako ambayo kila mara inakuletea mambo yasiyo na maana kabisa imefanya utafiti , je mbunge wetu angekuwa bunge jingine lenye lugha tofauti angesemaje? Nimekwepa kuweka tafsiri ya Kiswahili kwa kuwa wanaharakati watanibebea mabango......hebu tuendelee
Kispanyola- vete a la mierda
Kichina - 你他妈的
Kidenish -Fuck dig
Kifilipino - magkantot sa iyo
Kifaransa -  va te faire foutre
Kijerumani - fick dich
Kigujarat -  તમે વાહિયાત
Kitaliano -  vaffanculo
Kijapani -  性交
Kinorwiji - knulle deg
Kirusi -  пошел на хуй
 Kispanishi - vete a la mierda
Kiswidi -  knulla dig

16 April 2013

ILE CLIP YA MAZUNGUMZO YA SIMU YA MASUPASTA WAKIKATAANA IPO HAPA LAIVBI MKARIMU-SASA NIMECHOKA
Blog yako ya mambo yasiyo na maana yoyote imepata clip ya maongezi  yaliyorekodiwa ya masupata wa kisupasta, wakizungumza kisupasta umeonaee. Inshu nzima ilikuwa hivi, supatasta Mkarimu alimpigia simu supasta Pangalashaba. Kumbe Pangalashaba alikuwa na yule demu wake Sentitano, ambaye naye taratibu anapata usupasta kwa kuwa kampindua supasta na kuwa demu wa supasta, umenipataee. Ungepeeeeeeeeeeeenda kusikia mazungumzo yenye sauti za kisupasta?????????? Haya fungua masikio

Pangalashaba: Unajua mi sikufanyii drama, kiukweli mi nimembiliv huyu demu wangu Sentitano au vipi
Mkarimu: Haiwezekani, sasa halafu mimi je?
Pangalashaba: Bwana we tabu yako nikikula denda tu we unatangaza redioni, TV, KIU, Ijumaa mpaka polisi, so mimi niko na my baby full stop, unajua huyu msiri sana. Hata mimba yake watu hawajui kama anayo. (Sentitano si akaona heri anyang’anye simu
Sentitano: Hallo, wapi hapo? Haloooo
Mkarimu: Hmmmh
Sentitano: hallooooooooo
Mkarimu: Haloo Haloo ya Njenje kutia nazi kunoga
Sentitano: Halo sie tunataka kulala tunahitaji mtoto au vipi. Kitoto chetu kitakuwa nacho kisupasta mamy
Mkarimu: Jamani msilale kwanza
Sentitano: Baby wacha tulale ya?
Mkarimu: Mi sikubali msilale
Sentitano: Sisi tunalala
Mkarimu: Haiwezekani sasa mi nikalale na nani?
Sentitano: Hee utajiju shosti , sie tumeshamua kupendana na wewe tafuta wako
Mkarimu: Mbona mimi alinambia ananipenda, au alikuwa anatafuta Kiki kwangu, mi sikubali nyie wote mnanitafuta mnanisumbua kwa kuwa mi supasta, mnatafuta kiki kwangu. Dunia nzima hakuna supasta mzuri kama mimi, hata Obama ananijua
Sentitano: Mshikaji kalale sie tumekurekodi kila kitu na kesho tunasambaza kwenye daladala zote za mjini.
Baada ya clip hiyo kusikika Sunday Kahawia, yule Mbunge wa jimbo lisiloeleweka, alimpigia Mkarimu na kumuuliza juu ya mazungumzo haya…...

Mkarimu: Kwa kweli mi sijazungumza na mtu, watakuwa wamepesti kama walivyofanya yule mwanasiasa, like you see, me noo kabisa, I know this is because of kick start, wanataka kujulikana because I am supasta, watafute sehemu nyingine sio kwa mimi, sawa mi ninajijuwa me am a star, am a star like all over Tanzania hakuna star kama mimi sawa eeh, halafu we  Sunday mi nakuheshimu sana wewe, bahati yako au na wewe unataka kunichokonoa? Mi sitaki kuanza kuchokonolewa saa hizi, mi nimekaa tu kimya, am just quite na sijafanya kitu chochote am just quite, and am just going to stay quite, na usingenipigia simu mi ningeendelea kukaa kimya. Maana Kimya ni kukaa quite na quite ni kukaa kimya like I am silent
Sunday: Sikia bado unampenda Pangalashaba?
Mkarimu: What? Who is he? Ni nani huyo? Nilishampitia its over….
Bila hiana Sunday alitaka kubalans stori akaongea na Pangalashaba
Sunday: kwanini unamuonea mtoto wa watu wakati hakutaki hata kukuona?
Pangalashaba: Dah muongo huyo jana tu alikuwa ananibembeleza nimrudie mi ndio nikamuogopa mke wangu nikampa waongee kirafiki kama my baby atakubali powa, Baby wangu akasema tumrekodi tukapeleke kwenye BBM, ndio tukarekodi,

15 April 2013

HATA KWETU WAKOOOOO


NILIDHANI KASAFIRI

Mashosti walikutana asubuhi kwenye supu pale Garden Breeze, Shosti moja akatokea kavimba uso kwa kipigo.
SHOSTI 1: Hee vipi tena mwenzangu, yule bwana wa jana kakupiga?
SHOSTI 2: Mwenzangu, walaaa, kipigo hiki kanitandika mume wangu
SHOSTI 1: Jamani si mi nilijua mumeo kasafiri kenda Songea
SHOSTI 2: Hata mimi nilijua hivyohivyo

SIJUI KAMA BADO LINAUMA

GULO: Nilikuwa naumwa jino nikaenda kung'oa
FULO: Pole shosti vipi sasa bado linauma?
GULO: Mhhh sijui maana nilipoling'oa limebaki kulekule hospitali

14 April 2013

MNAOPENDA TATUU IGENI HAPA hahahahahahaah

Siku hizi imekuwa kama vile mjanja yoyote muhimu awe na tatuu. Haya igeni dizaini nyingine hizi hapa. Shenz type

11 April 2013

8 April 2013

BREAKING NYEUSSSSSIIIIII WADADA WAWILI WAUMANA MIDOMO HADHARANI

WADADA WAKIUMANA KWA HASIRA
Exclusive, breakiiing nyeusiiiiiii......blog yako ya makolokocho yaliyopitiliza imefanya utafiti wa hali ya juu kuhusu picha ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na isiyo ya kijamii dunia nzima kama vile cnnblogspot,bibisi na kadhalika, ikiwa na maelezo ambayo mtandao huu unayapinga kwa nguvu zote za giza. Utafiti uliofanywa na blog hii kwa kushirikisha mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu na yale ya hakimiliki imegundua kuwa watu wengi wanachokiona hapa sicho kilicho au tuseme kilicho sicho kilivyo, au tuseme kilivyo sicho ndicho, ushanijua ee. Kwa kutumia utaalamu wa hali ya juu sana ambao utaalamu huu ulitumika katika kufanya utafiti wa kugundua kama Saddam Hussein ana mabomu ya nyuklia mfukoni au la, na utaalamu huu ulitumika pia katika kutafuta gesi Ntwara, mtandao huu na washirika wake wamegundua mambo kadhaa yaliyokuwa yakitokea wakati wa kupigwa kwa hii picha. Kwa kupitisha kwenye International Chinese Analogue Digital Scanner(ICADS), imeonekana picha hii ni feki, lakini baada ya kuiscan kwenye Mobile Colour Text Scanner(MCTS) ikaonekana kuwa kulikuwa na kelele za watu wengi wakati picha hii inapigwa, na pia kulikuwa na harufu za pafyum mchanganyiko na udi wa Zanzibar. Hii ilisaidia kucreate atmosphere ambayo ilileta mitandao mingi kuona kile ambacho kiukweli kilikuwepo hakipo. Utafiti huu umegundua kuwa picha hii inaashiria kulikuwa na ugomvi mkali kati ya wanaonekana katika picha maana hapa walifikia hatua ya kutaka kuumana kwa hasira kali iliyokuwa imewazidi, lakini kumbe mmoja alikuwa katoka kula mishkaki yenye pilipili iliyowafanya wote wafunge macho kwa uchungu wa pilipili hiyo. Uchunguzi pia umegundua kuwa katikati ya hawa wadada kuna mdada mwingine aliyekuwa nyuma yao, ambaye ni wazi anatumia mkorogo wa hali ya juu, kwani vidole vyake tu vilivyoshika glasi ya ulanzi vinaonekana vikiwa vimeathirika na mkorogo. Mtandao huu unaendelea na upelelezi kujua je ugomvi huu uliishia wapi? na je, kuna mtu labda alinyofolewa midomo au ulimi?. Fuatilia mkasa mzima kwenye blog hii yenye watafiti waliobobea ambao kauli mbiu yetu ni..... unaweza kukwepa mvua lakini sio utafiti wetu.
Mkurugenzi Mwenye Enzi

WATANZANIA TUMEKUWA WA 6 KWA KUKATAA POMBE ZA KUZUNGU
Utafiti wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kukataa kunywa pombe za kigeni (mawhisky, mabrandy, mabia na uchafu mwingine).

Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe walioipenda ijulikanayo  kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.

Kwa mujibu wa utafiti huo,Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52,ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07. Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa za asili.

Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.

Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa , eti  aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo zenye historia ndefu kwa sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama kwa wazungu.

Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya za wageni watakaoonja pombe hizo.“Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini,moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza, lakini hakusema kuwa jambo  hili pia linatokea kwa pombe za kizungu.

Dk  pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo, inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” Japo wote tunajua kuwa kusahau ni aina ya kupunguza mawazo.
Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya. Kwa mfano kama huna ada ya shule kwa wanao nenda kituo cha afya upate ushauri nasaha, utaondoa msongo.
 
Katika miaka ya hivi karibuni,kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine. Hapa tunazungumzia pombe za kiafrika tu za kizungu kunyweni ni safi zana kwa kuondoa msongo wa mawazo.

6 April 2013

BREAKING NYEUSSSSSSI....SHABIKI WA BLOGGERS FC AKITOA USHAURI NASAHA KWA REFA

Shabiki maarufu wa Bloggers FC alilazimika kutoa ushauri wa hali ya juu kwa refa wa mtanange huu baada ya soka kali lilionyeshwa na vijana wadogo wa chini ya miaka 18 wa Bloggers FC. Tulipojaribu kumpigia simu shabiki huyu ili tujue nini kilijiri hapa, simu yake ilijibiwa na mwanamke mmoja ambaye hakujitambulisha aliyejipendekeza na kuanza kujibu.."Namba unayopiga inatumika usikate kiuno bonyeza chochote.." jambo lililomuudhi mwandishi wetu na akakata simu kwa hasira

BLOGGERS FC YAFANYA MAAJABU MZEE WA TIMU AKESHA KWENYE PIPA LA KOMONI

Leo ilikuwa siku kubwa sana kwa wana media mbalimbali hapa Dar es Salaam, kwani katika viwanja vya Leaders mamia ya wanamedia na wadogo zao, watoto wao, ndugu zao, na jirani zao walikusanyika katika viwanja hivi na kukawa na mashindano ya michezo mbalimbali. Katika mashindano hayo mchezo uliovutia kuliko yote ni ule wa soka kati ya Bloggers FC na timu iliyokusanywa harakaharaka ya Radio Maria FC. Bloggers FC ni timu ngeni kabisa katika ulimwengu wa soka lakini ilikuwa na wachezaji wenye kufanana kwa mambo mengi na wachezaji kutoka timu za Divishen ya kwanza Italia, Spain, Uingereza na Brazil, kifupi timu hii ilikuwa na majembe kama sio sululu kabisa. Timu hii ambayo ilifanya mazoezi makali kwa dakika chache kabla tu ya kuanza kwa mechi, ilifungwa kwa taabu saana katika mchezo wa raundi ya pili ya ligi, kwa magoli matatu bila na timu ndogo ya Radio Maria.
Miguu ya wachezaji:
Zifuatazo ni picha miguu ya majembe hayo, katika hii picha ya kwanza  ni miguu hii hakuna shaka  ni kama Rooney ila sema ya hii  mieusi kidogo, nadhani huyu ni www.othmanmichuzi.blogspot.comKatika raundi ya kwanza timu moja pinzani (jina linahifadhiwa kwa leo), baada ya kuona aina ya miguu ya wachezaji wa Bloggers FC, ilikataa katakata kuingia uwanjani na hivyo kuipa ushindi timu hii tishio. Mtaalamu mkazi au tuseme Mzee wa kamati ya ufundi ya timu  alilazimika kwenda Iringa Vijijini kuchukua zana za kazi kuhakikisha ushindi, huyu si mwingine ila ni blogger maarufu wa Blog isiyo na maana yoyote duniani ijulikanayo kama www.chekanakitime.blogspot.com ,maarufu kwa jina la ajabu Mzee Kitime.
Mzee huyu ambaye alilazimika  kukesha kwenye pipa la pombe maarufu iitwayo komoni hii ni kusaidia timu pinzani zijisikie zimelewa komoni wakati zikiwa zinacheza na Bloggers FC, bahati mbaya alikosea masharti na kunywa soda kabla ya mechi jambo lililofanya timu yake ndio ikalewa na kujikuta imefungwa 3-0 na Radio Maria FC. Lakini baada ya kukimbia  na kufanya kafala fulani chini ya Mbuyu ulioko Kenyatta Drive mambo yalikubali na Bloggers FC wakaitandika timu ya DSJ 3-2 na kuingia fainali. Katika hali ambayo ilimshangaza hata mtaalamu aliyekuwa akimsaidia Mganga wa timu, eti ushindi ikapewa timu ya Mwana nchi FC, ushindi wa pili ikapewa Radio Maria FC na Bloggers FC eti ya tatu. Any way shukrani kubwa kwa wadhamini wa Bloggers FC  SAPPHIRE COURT HOTEL ya Jijini Dar