HATUPIMI BANDO

26 March 2013

BREAKING NEWS MASHINE YA KUPIMIA UJINGA YAINGIA NCHI KWA KISHINDO

HATIMAYE SERIKALI ILE SIKIVU IMESIKIA KILIO CHA WANANCHI NA KUNUNUA MASHINE ZITAKAYOWEZESHA KUTUMIKA KUPIMIA KIWANGO CHA UJINGA KATIKA SEKTA , KAMPUNI NA WIZARA MBALIMBALI. KWA KUANZIA KUNA MPANGO MKAKATI WA KUPIMA WAENDESHA BODABODA WOTE, ILI KUWA NA TAKWIMU YA KIWANGO CHAO HII ITASAIDIA KATIKA KUTAFUTA MBINU ZA KUPUNGUZA AJALI. PIA WANANCHI WENGI WAMEITAKA KAMPUNI MOJA YA SIMU KUWA IPIMWE KUANZIA KAMPUNI YENYEWE NA WATUMISHI WAKE WOTE, WALE WA KASTAMA SEVIS YA KAMPUNI HIYO WATAPIMWA MARA MBILIMBILI. KISHA KUTAKUWEKO NA MPANGO WA KUHAMIA KATIKA WIZARA MBALIMBALI HAPA KUTOKANA NA KUZUIA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA SITATAJA HIZO IDARA. KAMPUNI KAMA ILE YA KUWASHA GIZA ITAHUSIKA SANA. KWA SABABU ZA KIMSINGI MASHINE MBILI ZITAKUWA DODOMA KATIKA KIPINDI CHA BUNGE KWA AJILI YA MATUMIZI YA KAWAIDA.

1 comment:

Musa Kitonge said...

Hatuhitaji mashine sisi tumeshaukubali ujinga wetu tutakufa nao