HATUPIMI BANDO

31 March 2013

HA JAMANI WABONGO WEZI WAMEIBA MPAKA....

They have stolen my iPhone, nilikuwa nayo sasa hivi, Wabongo wezi sana, mi sikubali haaa

28 March 2013

BREAKING NYEUSIIII>>>>Baby Nakupenda kupita maelezo

MDADA:Hello sweety
MKAKA: Hello mambo baby?
MDADA: Poa nikuulize kitu?
MKAKA: Uliza baby
MDADA:Unanipenda?
MKAKA: Sana tu
MDADA: Unanipenda kiasi gani?
MKAKA: Yaani hakuna mfano
MDADA: Sema tu kiasi gani
MKAKA: Nakupenda kupita maelezo na nitakupenda daima hata kitokee nini
MDADA: Ok
MKAKA: Kwanini lakini umeniuliza haya?
MDADA: Nimeuliza tu
MKAKA: Mhh lazima kuna kitu 
MDADA: Ahh we acha tu
MKAKA: Sema baby unajua nakupenda
MDADA: Nadhani nina mimba
MDADA: Haloo, haloo haloo sweety unanisikia? Sijui netwek? Simu imekatika ghafla
 

27 March 2013

WANAKULA RUSHWA

Jamaa kaandika kwenye gari lake, 'TRAFIKI WANAKULA RUSHWA'. Haukupita muda Trafiki wakamkamata na baada ya kipigo kizuri tu akalipa 'faini-pori' akaachiwa kwa masharti kuwa akafute maandishi.
Jamaa akafuta maandishi yale lakini akaandika mengine'BADO WANAENDELEA KULA'

26 March 2013

BREAKING NEWS MASHINE YA KUPIMIA UJINGA YAINGIA NCHI KWA KISHINDO

HATIMAYE SERIKALI ILE SIKIVU IMESIKIA KILIO CHA WANANCHI NA KUNUNUA MASHINE ZITAKAYOWEZESHA KUTUMIKA KUPIMIA KIWANGO CHA UJINGA KATIKA SEKTA , KAMPUNI NA WIZARA MBALIMBALI. KWA KUANZIA KUNA MPANGO MKAKATI WA KUPIMA WAENDESHA BODABODA WOTE, ILI KUWA NA TAKWIMU YA KIWANGO CHAO HII ITASAIDIA KATIKA KUTAFUTA MBINU ZA KUPUNGUZA AJALI. PIA WANANCHI WENGI WAMEITAKA KAMPUNI MOJA YA SIMU KUWA IPIMWE KUANZIA KAMPUNI YENYEWE NA WATUMISHI WAKE WOTE, WALE WA KASTAMA SEVIS YA KAMPUNI HIYO WATAPIMWA MARA MBILIMBILI. KISHA KUTAKUWEKO NA MPANGO WA KUHAMIA KATIKA WIZARA MBALIMBALI HAPA KUTOKANA NA KUZUIA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA SITATAJA HIZO IDARA. KAMPUNI KAMA ILE YA KUWASHA GIZA ITAHUSIKA SANA. KWA SABABU ZA KIMSINGI MASHINE MBILI ZITAKUWA DODOMA KATIKA KIPINDI CHA BUNGE KWA AJILI YA MATUMIZI YA KAWAIDA.

18 March 2013

BREAKING NYEUSIIIIIIIIIIII MATANGAZO YA KAZI


Kuna matangazo ya kazi yametolewa Kiingereza, sasa nakupa tafsiri yake kisirisiri usimwambie mtu

1.  Landscape Executive and Animal Nutritionist
- Shamba Boy 
2. Domestic Operations Specialist -
Haus gelo
3. Printed Document Handler -
Typist
4.  Regional Business Communications Conveyer -
Mesenja 
5. Transparent Wall Technician -
Msafisha madirisha
6.
Associate Tutor - Mwalimu wa Twishen

7. Refreshments Overseer -
Mhudumu wa Chai
8. Public Sanitation Technician -
Mzoa taka
9.  Area Theft Prevention and Surveillance Officer-
Mlinzi  
10.  Office Access Control Specialist -
Receptionist
13.  Food Technician and Preparation Officer -
Mpishi  .

ASKOFU KITIME DAH!!!!!


Nimemkuta rafiki yangu analia kama mtoto mdogo chumbani kwake;
MIMI: Oya mshkaji vipi tena nani kafa?
MSHKAJI: Yaani Gulo kaniuwa, hivihivi bila kosa kaniuwa
MIMI: Hebu tulia nambie ishu nzima
MSHKAJI: Si unajua nimekuwa namlipia Gulo ada toka sekondari mpaka sasa yuko chuo nikijua ndio niko peke yangu na nitamuoa?
MIMI: Ndio
MSHKAJI: Jana nikataka kuangalia kanisevu nini kwenye simu yake
MIMI: Ok
MSHKAJI: Si kanisevu eti Mchungaji Peter 12
MIMI: Sasa tatizo liko wapi
MSHKAJI: Nilipoangalia majina mengine sinimekuta kuna Pasta Hamfrey, Pasta Henry, Askof Kitime , na kuna Mchungaji Peter 1 mpaka mimi wa 12, wakati  hata siku moja haendi kanisani wala maombi
MIMI: Dah endelea kulia mwanangu

15 March 2013

YAMENIKUTA


BREAKIIIIIIIIIIIIIIING POINT..SABUNI YA KUFUKUZIA MASHETANI


VINYAMUZI, EH VISAMBUZI, EH VING'AMUZI

KWA katuni nyingi zaidi ingia hapa uone kazi za Marko marcotibasima.blogspot.com/

KWELI? AU KUSUDI NISIKIE WIVU?

MAMA: Unajua huyu babako nina wasiwasi ana uhusiano na sekretari wake kazini,
HAUSGELO: Mama una uhakika au unasema tu kusudi nisikie wivu?

NIKUPE TOOTHPICK?

Ulitoa mchango wako mkubwa kwenye vikao vya harusi, sasa siku ya harusi unapanga foleni ya chakula, inapofika zamu yako chakula kinaisha, unarudi mezani kupata kinywaji unaambiwa vinywaji vimeisha, wakati unawaza kwa masikitiko kuhusu  mchango wako, mhudumu anapita ana kuuliza, 'Samahani mzee umeshakula nikupe toothpick?'

13 March 2013

MAMA MKWE SIMTAKI MWANANO

JAMAA: Mama mi na mwanao basi, nimechoka
MAMA MKWE: Kwani vipi mkwe?
JAMAA: Nilikuwa safari nimemtumia mke wangu ujumbe kuwa niko njiani narudi, eti kanidharau kiasi nimemkuta na bwana chumbani kwangu simtaki tena
MAMA MKWE:Tulia jamani, mbona hicho kitu kinanishangaza hiyo wala si tabia ya mwanangu, ngoja nimuulize kimetokea nini......................................
MAMA MKWE: Unaona baba unaona mi nilisema lazima kuna sababu, ona mwenyewe kumbe meseji uliyotuma ndio kwanza imeingia.

BABA MI NIMETOKA WAPI?

DOGO: Eti baba mi nilitoka wapi?
BABA: Dah, unajua mwanangu umeuliza swali zuri sana, kimsingi, ni mefurahi kuwa umeuliza, sasa eh eh eh sasa yaani mi na mama yako tulifahamiana kwanza kwenye facebook, hatimae tukakutana faragha ndio babu yako akatulazimisha tuoane ndio baada ya miezi michache wewe ukaja, sijui umeelewa nadhni
DOGO: Wala sijaelewa, mwenzangu Gulo kasema yeye katoka Songea, sasa mimi nimetoka wapi sijui

11 March 2013

PIKA UGALI

Mmama kaenda polisi;
MMAMA: Kuna tatizo, mume wangu ameondoka nyumbani toka jana akanambia anaenda sokoni, kununua viazi na hajarudi mpaka leo. Naomba mnisaidie
POLISI: Kwani huwezi kupika ugali?

NAMPIGA MAMA

Mtoto kwa bahati mbaya kaingia chumbani kwa wazazi wake kawakuta wako faragha.
MTOTO: Baba mnafanya nini?
BABA: Nampiga mama
MTOTO: Mama umefanya nini leo? Anko Jelo kakupiga, Dreva kakupiga, Muuza magazeti kakupiga, sasa baba anakupiga, umezidi wewe

9 March 2013

BREAKING NYEUSSSSSSSI- ARSENAL WANA SAHANI NYINGI TU PIA

 Tunategemea baada ya uchunguzi huu, watu watafungwa midomo kuhusu Club kubwa la Arsenal. Arsenal wana vikombe kibao na si hilo tu pia wana sahani, nyie Yanga na Simba  mna sahani? semeni  ah ah mnasahaniii?BREAKING NYEUSSSSSSSSSSSI ...ARSENAL INA VIKOMBE VINGI TU

Kuna watu wana majungu sana wanaeneza hadithi eti Arsenal haina vikombe. Kamati ya uchunguzi ya blog hii imegundua kuwa hilo si ukweli na tumeamua kuliweka wazi kwa ulimwengu wote kuwa Arsenal wanavikombe tena vingi tu, na hivi sasa tunaangalia uwezekano wa kufanya utafiti kama pia wana sahani. Arsenal Hoyeeeee

KICHEKESHO TOKA KENYA ...MAJUKUMU YA RAIS MPYA

WAKENYA TUNATAKA PRESIDENT IKO NATIMIZA MABO HAYA:-

1. Introduce petrol ya satchet kwa watu wa vitz
na probox..(no offense)

2. Wapunguze bei ya mutura na mahindi choma
juu wanatumia gas kuchoma.

3. Siku za mwizi ziongezwe from 40 to 70 juu
kumekauka.

4. Bei ya iphone ireduce juu mtu alishaa bite
hiyo apple.

5. Tissue paper itolewe hiyo second sheet.
(inakuwanga ya nini by the way?)

6. Ile light huwanga "at the end of the tunnel"
izimwe to save energy.

7. Ma subscribers wa Safcom wote warudishiwe
hiyo "bob" ikokwa jina la Collymore. Huyo
jamaa anakula bob kwa kila subscriber, siyo poa,
inafaa abaki tu Collymore.

8. Miguna Miguna anyanganywe jina moja
wapatie wenye hawana majina kama Nameless.

9.Gava ifungue Mr. Broke coz hatuwezani na Mr.
Price

10. Bei ya doughnut ibaki vilevile but wapunguze au wazibe ile
shimo

11. Bei ya soda ipunguzwe coz haikuwangi imejaa
ama wajaze

12. The road to success ikuwe super highway ndio
wasee wafike haraka

13. Atoe remix ya national anthem iwe na beats za Heart & Soul riddim.

14. Wapunguze fare ya kwenda S.africa kwa ndege juu ni mteremko ndege haitumii mafuta

8 March 2013

NANI FALA ZAIDI?

BABA: Sikiliza Dogo akija mtu kunitafuta mwambie nimesafiri
DOGO: Sawa  baba...............
MGENI: Dogo baba yako yupo?
DOGO: Baba kasafiri
MGENI: Kaenda wapi?
DOGO: Ngoja nikamuulize................
DOGO: Mgeni anauliza umesafiri umeenda wapi?
BABA:Mwambie nimeenda Songea.........
DOGO: Baba kasema ameenda Songea.
MGENI: Basi akirudi mwambie anitaarifu

BABA NIMERITHI AKILI KWA NANI?

DOGO: Eti baba mimi akili nimerithi kwanani?
BABA: Itakuwa umerithi kwa mama yako mimi zangu bado ninazo

1 March 2013

HUYO NGURUWE UMESHAMTOA?


Jamaa alikuwa baa anakunywa, rafiki yake akaja wakawa katika mazungumzo;
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja nauliza, "Huyo nguruwe umeshamuondoa?' Yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka

CHEZEA MSWAHILI WEWEEEEE