HATUPIMI BANDO

2 February 2013

UJUMBE KWA WACHORA KATUNI aka MAKAVU LAIVU YAO

Halo, tafadhali ujumbe huu unawahusu wachora katuni aka wachora vibonzo. Hebu simameni kwanza niwaone wote. Masoud, Marco aka Ka-kobe, Aloys, Kakakeri, Twalipo, Katembo, mLevy, Nko, okay, wengine wako wapi?,King Kinya yuko wapi? ohh kwenye GESI? (Nimesema gesi siyo gesti, msinianzishie bifu na best wangu)
Poa. Sasa hivi nyie watu mnajua matatizo ambayo mnaniletea? Hivi mnaona ni sawa kabisa kuweka vibonzo ambavyo vinasababisha mi niwe nacheka hovyo kwenye vihais kama mwehu? Why men? Mtu unakuwa na akili gani kufikiria kibonzo eti mtu akichanganya mno vyakula ataota kaolewa, je hiyo ndio sera inayoweza kuleta maendeleo kwa sisi vijana wa kizazi hiki? Kwanini hamchori mambo ya kimaendeleo kama mashamba ya Ujamaa na kujitegemea au usafi wa Kinondoni au kilimo cha kufa na kupona au gesi…..ehhh hapana msichole gesi itakuwa soooo, yaani choleni mambo ya maana, ili niweze kujizuia kununua magalizeti mengi kwa mpigo ili nisikose mipicha yenu ya ajabu ajabu. Kumbukeni vitabu vya wahenga vilisema CHEKESHENI NANYI MTACHEKWA, ohoooo nyie haya. Kuanzia kesho mkinichekesha naenda kuchoma moto nyumba za wabunge wenu.

No comments: