PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NYOTA ZENU...usiachike bure soma nyota zako

Kwa kweli huwa sipendi sana kutumia utaalamu wangu wa nyota lakini kwa maombi ya wengi nimelazimu kuchukua nafadsi hii kutabili mambo muhimu katika kipindi cha wiki mbili zijazo
Kuanzia leo tarehe 2 February hadi 15 Februari ni kipindi kibaya kwa wapendanao. Kuna wadada wengi watajikuta wanaachika bila sababu maalumu, kitendo cha kumtania umpendae kitaishia kufukuzwa kwa hasira kuu, hii ni kutokana na nyota kuingiliana njia. Bahati nzuri ni rahisi sana kukwepa balaa hili la kuachika. Wadada ni muhimu nasema ni muhimu, kuanzia leo, usitamke neno VALENTINE. Kwa kuwa kinyota neno hilo limezingirwa na nyota nyeusi isiyotabilika na hivyo kuweza kumfanya mpenzi wako asitabirike na kukufukuza bila sababu. Epuka narudia tena epuka kutamka neno VALENTINE na hasa ukuwa umeunganisha katika sentensi moja neno ZAWADI. Balaa hili litapita tarehe 15 asubuhi, hapo unaweza kutamka neno hilo bila balaa yoyote. Ila kwa wale wataakaoachika wasipaniki maana nyota zinaonyesha mambo yatarudi katika hali yake kuanzia hiyo tarehe 15.

Comments