PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NYANI DREVA WA GARI LILILOPATA AJALI


Trafiki kakuta bonge ya ajali, dereva na pasenja mwanamke wamefariki. Wakati akiangalia angalia kakajitokeza kanyani, toka uvunguni mwa gari kakawa kana ruka ruka. Trafiki akasema, ‘Ungekuwa unajua kuongea si ungetuhadithia ilikuwaje’ Nyani akatikisika kichwa kuonyesha kaelewa. Trafiki akauliza, ‘Ilikuwaje?’.  Nyani akaokota kopo la bia na kuonyesha ishara ya kunywa, polisi akasema ‘ Walikuwa wanakunywa?’ Nyani katikisa kichwa kukubali. Halafu nyani akaonyesha ishara ya kuvuta sigara, askari akauliza, ‘Walikuwa wanavuta bangi?’  Nyani akatikisa kichwa kukubali, Polisi akauliza ‘Na nini kingine?’ Nyani akaonyesha ishara kuwa walikuwa wanabusiana, ‘ He walikuwa wanabusiana pia?’  Nyani kakubali. Polisi akauliza, ‘Sasa wakati wanakunywa pombe, wanavuta bangi, na kubusiana we ulikuwa wapi?’ Nyani akaonyesha ishara kuwa yeye ndiye alikuwa anaeendesha gari.

Comments