HATUPIMI BANDO

6 February 2013

KASHESHE ZA MESEJI ZA SIMU


Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;
Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
Simu  2- He Mama Joji unaumwa?
Simu 3- Nami pia daima
Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe
Simu 8-Chukua taim yako
Simu 9-?!?
Simu  10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?
Simu 11 – Hivi naota?
Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi mkubwa
Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi

1 comment:

MAKALA ZANGU said...

Duu. Tamu hii, Kitime. Inachekesha na mafunzo kem kem ndani. Watu tusioaminiana. Somo la kwanza. Mwenendo usiozeleka kiutamaduni.Pili, ni swali. Je, kidesturi siye Waswahili huonyeshana mapenzi kwa vitendo au kwa maneno? Mi binafsi naamini matendo huongea vyema zaidi kuliko bla bla...na ndiyo sababu hao waume wenzangu hawakuamini kauli!