PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

JANA ILIKUWA HOVYO, JANA ILIKUWA FRESH

Wake wawili walikutana kazini;
MKE 1: Vipi shosti za toka jana?
MKE 2: Hovyo kabisa. Nimetengeneza chakula, jamaa limerudi limelewa, likala chakula bila hata kuongea likakaa kwenye kiti na kupitiwa na usingizi maudhi matupu
MKE 1: Mimi ilikuwa raha, mume wangu alinitoa out, halafu tukarudi home tunatembea kwa miguu, tulipofika home, akawasha mishumaa nyumba nzima ilikuwa sooo romantic.
Waume zao kumbe nao wamekutana.......
MUME 1:Vipi kwako mkuu?
MUME 2: Ilikuwa safi sana, nimerudi home na kilaji kichwani nikamkuta jamaa amepika nikala nikalala fofofo.
MUME 1: Kwangu hovyo, nimerudi home umeme hakuna, chakula hakuna nikalazimika kutoka na waif tukatafute msosi, tumemaliza kula nimelipa si nikagundua nimechukua hela kidogo nikawa sina hata nauli ya taxi,ikalazimika kurudi home kwa mguu, umeme ukawa bado haujarudi nikalazimika kuwasha mishumaa nyuma nzima yaani hovyo kabisa.

Comments