PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

HUYU MJANE MZEE ANAKAA WAPI?


Jamaa: Mjomba nina jambo linanizingua.
Mjomba: Nini tena nambie
Jamaa: Nataka kuoa sasa nina wapenzi wawili, wa kwanza ambaye ndiye moyo wangu unampenda ni msichana mzuri lakini masikini, wa pili ni bibi moja mjane mzee lakini tajiri, nifanye nini mjomba?
Mjomba: Fwata moyo wako mjomba wangu, muoe unaempenda mjomba wangu.
Jamaa: Yaani mjomba asante kwa mawazo mazuri , hata mimi nilikuwa nafikiria hivyohivyo,
Mjomba: Sasa umesema huyo mjane mzee anakaa wapi?


Comments