PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

CHONDE CHONDE NAOMBA USHAURI

Mzee Kitime tafadhali naomba ushauri katika hili tatizo langu. Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi katikati ya jiji, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi na taxi wakati najua mshahara wake hautoshi kugharamia hilo, wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu yake alikuwa mkali kwelikweli kidogo aniue. Ni kweli sijawahi kumuonyesha dalili zozote zaidi kuhusu wasiwasi wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, nikaona niangalie saa ili nijue ni saa ngapi walitoka, si ndio nikagundua saa yangu imesimama, saa hii saa yangu ni Rolex na saa za aina hii ni expensive sana, alinitumia rafiki yangu toka Uswisi na kunambia ina gerentii haitasimama kamwe, sasa unanishauri vipi, niitengeze hapa nchini, au nimrudishie itengenezwe Uswisi au ninunue nyingine?

Comments