HATUPIMI BANDO

28 February 2013

WE MDADA VIPIIII?


HUYU MJANE MZEE ANAKAA WAPI?


Jamaa: Mjomba nina jambo linanizingua.
Mjomba: Nini tena nambie
Jamaa: Nataka kuoa sasa nina wapenzi wawili, wa kwanza ambaye ndiye moyo wangu unampenda ni msichana mzuri lakini masikini, wa pili ni bibi moja mjane mzee lakini tajiri, nifanye nini mjomba?
Mjomba: Fwata moyo wako mjomba wangu, muoe unaempenda mjomba wangu.
Jamaa: Yaani mjomba asante kwa mawazo mazuri , hata mimi nilikuwa nafikiria hivyohivyo,
Mjomba: Sasa umesema huyo mjane mzee anakaa wapi?


SIRI IMEFICHUKA...msanii wa bongomuvi 2020

Wataalamu wa IT wameweza kubuni taaluma ambayo inaonyesha mtu atakuwaje miaka kumi kutoka leo. Na hapa ni picha ya superstar wetu maarufu wa Bongo Movie atakavyokuwa baada ya miaka 7. Kutokana na unyeti wa jambo lenyewe hatutamtaja msanii huyu mpaka tutakapowasiliana nae, kwa muda huu simu yake haipokelewi labda yuko shuting.

POLE NDO TABU YA UROJO


CHONDE CHONDE NAOMBA USHAURI

Mzee Kitime tafadhali naomba ushauri katika hili tatizo langu. Mi nadhani mke wangu si muaminifu, anafanya kazi katikati ya jiji, huwa anachelewa kurudi nyumbani na kila siku anarudi na taxi wakati najua mshahara wake hautoshi kugharamia hilo, wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu yake alikuwa mkali kwelikweli kidogo aniue. Ni kweli sijawahi kumuonyesha dalili zozote zaidi kuhusu wasiwasi wangu, lakini jana nilamua kumfuatilia wakati anatoka kazini, nikajificha mahala ambapo ntamuona anapotoka kazini, kweli nikamuona anatoka na mwanaume mmoja simfahamu, nikaona niangalie saa ili nijue ni saa ngapi walitoka, si ndio nikagundua saa yangu imesimama, saa hii saa yangu ni Rolex na saa za aina hii ni expensive sana, alinitumia rafiki yangu toka Uswisi na kunambia ina gerentii haitasimama kamwe, sasa unanishauri vipi, niitengeze hapa nchini, au nimrudishie itengenezwe Uswisi au ninunue nyingine?

24 February 2013

Breaking Nyeusi!!!!!!!Bibi harusi atinga kwake na mizigo

Sawa kabisa njoo na mzigo wako wakuanzia maisha. Nani kasema kila kitu kiko kwa mwanaume? Anamelemeta anamelemeta

BARUA TOKA KWA MTAHINIWA FORM 4


Good morning Sir,
Pliz my name is ************ I am finish fom for. Ze everybody is to say we get za divishen 0, My part I am saying not I am not get divshen 0. I am vere vere intelijens, but pipoz don’t like me. I have experience in singing bongoflava, so pipoz are jelas, the have put majik so I get diveshen 0. But I am clever becoz ask me forekzampo, what is fomula for water? Ze fomula for water iz Hech to o. Now why you give me dishen 0? Ok ask me anadha forekzampo what iz President of America? Ze president of America iz Obama.  Ze gavament shud change my marks to dishen 2, because the youth are ze future of my country. If we get divishen 0 zen all the future is divishen 0. So giv us more  maks becoz of ze future
Pliz mzee put on ze facebook so ze Plezident will see

BREAKING NYEUSIIIIIIIIIIIIII----MJUMBE AMTANDIKA CHAKUBIMBI NGUMI MFULULIZO

Bila kipigo humu ndani kunakuwa hakuna heshima kabisa chukua hiyoooooooo

PICHA YAKO 'LIVE' KANIPA MJOMBA WAKO


UNAPOSAHAU SIMU NYUMBANI

Jamaa alikuwa njiani anaenda kanisani, si akashtuka kukumbuka kuwa ameacha simu yake nyumbani. Haraka akageuza njia na kuanza kurudi  nyumbani, alipofika home presha ikiwa juu bahati nzuri akauta mkewe hajaamka akaichukua simu yake na kuvunja safari ya kwenda kanisani akaanza kuangalia TV, mkewe alipoamka akamkuta jamaa kajaa tele sebuleni,
MKE: Jamani si nilidhani umeenda kanisani?
JAMAA: Mchungaji kanitext kasema leo hakuna ibada.

MBWA KOKO AWASIFIA MBWA WA POLISI

Mbwa koko wawili walikuwa wanasaka chakula kwele jalala, mara ikapita Land Rover ya FFU na ndani yake kuna mbwa wa polisi;
Mbwa koko mmoja akaangalia kwa uchungu kisha akamwambia mwenzie, ' Unaona wenzetu waliosoma, wale wanaenda kazini'

SWALI LA FOM FO

Fom fo ya kibongobongo;
Q 1. Describe a cow;
Jibu toka kwa fom fo;
He is the cow. He has 4 legs together 2
towards and 2 afterwards It gives milk
which comes from 4 holes on
the bottom.
He is mostly a girl. Its loose motion is
very useful,green colour.
It has tail situated in the backyard and
has hair on it to frighten flies.
Many use it as a vehicle also. He dies
after death.

23 February 2013

zhen feu zhech

Janfoi chu Li xu huan zhen feu zhech feng Lee.  Ming yao yeng kong hong king? Ming hao shu wein shao shing xhen yui wa.. Na kwa hiyo ndio hivyo tena, tukajikuta tuko kituoni mizigo yote imechukuliwa. Tsan kung fe ming tao li shi shuan Tanzania. Ndo Fulo aktoa msaada wa nauli, Gulo shing wha fung fung li , yaani hamna kitu kabisa, anyway tuko poa  sasa

19 February 2013

JANA ILIKUWA HOVYO, JANA ILIKUWA FRESH

Wake wawili walikutana kazini;
MKE 1: Vipi shosti za toka jana?
MKE 2: Hovyo kabisa. Nimetengeneza chakula, jamaa limerudi limelewa, likala chakula bila hata kuongea likakaa kwenye kiti na kupitiwa na usingizi maudhi matupu
MKE 1: Mimi ilikuwa raha, mume wangu alinitoa out, halafu tukarudi home tunatembea kwa miguu, tulipofika home, akawasha mishumaa nyumba nzima ilikuwa sooo romantic.
Waume zao kumbe nao wamekutana.......
MUME 1:Vipi kwako mkuu?
MUME 2: Ilikuwa safi sana, nimerudi home na kilaji kichwani nikamkuta jamaa amepika nikala nikalala fofofo.
MUME 1: Kwangu hovyo, nimerudi home umeme hakuna, chakula hakuna nikalazimika kutoka na waif tukatafute msosi, tumemaliza kula nimelipa si nikagundua nimechukua hela kidogo nikawa sina hata nauli ya taxi,ikalazimika kurudi home kwa mguu, umeme ukawa bado haujarudi nikalazimika kuwasha mishumaa nyuma nzima yaani hovyo kabisa.

18 February 2013

MITIHANI YETU WACHA WEWEEEEE

KICHAA BIN UCHIZI

Kichaa ni pale unapopata txt toka kwa mswity wako wa maisha inasema,' Sweety mi nimechoka naona tuachane', uchizi ni pale inapofuatia txt nyingine, 'Sorry love hiyo txt siyo yako'

YULE NI MIMI NAENDA KAZINI

Jamaa alionekana kapona hivyo atolewe kwenye hospitali ya machizi arudishwe kwao. Asubuhi mmoja akachukuliwa na ambulance mpaka jirani na kwake, akaulizwa unapafahamu hapa? Akajibu ' Ndio nyumba yangu ileee". Ghafla mlango wa nyumba ile ukafunguka wakatoka watoto wawili wamevaa yunifom,'Hee na watoto wangu walee wanaenda shule'. Mara akatoka mwanamke, jamaa akafurahi,' Mke wangu yule, mke wangu jamani'. Madaktari walianza kumfungulia atoke kwenye gari ghafla mwanaume akatoka kwenye ile nyumba, jamaa akaangalia kwa makini kisha akaruka kwa furaha,' Mimi yulee naenda kazini, unaona nilivyopendeza na suti ile nilinunua Mariedo'. haraka sana akarudishwa hospitalini.

SABABU YA NYANI KUKOSA NGOZI MAKALIONI

Hadithi hadithi, hapo zamani kidogo mbwa alikosea njia akaingia mbuga ya wanyama ya Serengeti, simba akamuona kwa mbali akajisemea, 'Haka tena kanyama gani? Ngoja nikaonje labda katamu'. Akaanza kukasogelea kambwa, mbwa ghafla akamuona simba akahisi hatari, akataka kukimbia ghafla akaona mifupa mbele yake akainama akaanza kujifanya anatafuna, huku akijisemea, 'Dah nyama ya simba tamu sana', simba kusikia hayo akashtuka akajua haka kamnyama kashenzi. Akaanza kuondoka taratibu kakunja mkia. Nyani alikuwa juu ya mti alikuwa kaona mchezo mzima, akaona hapa ndio mahala pa kujipatia mihela toka kwa simba, akamuwahi simba na kumwambia 'Bwana mkubwa ee unaogopa bure, nifwate mimi ukale kale kanyama'. wakati wanakuja mbwa si akawaona akajua mambo yameharibika, walipokaribia mbwa akajidai hajawaona ila amekasirika,' Huyu nyani yuko wapi, sinilimtuma aniletee simba mwingine?'. Duh simba kusikia hivyo akamkwangua nyani nyuma kwa hasira na kutokomea porini. na ndio maana mpaka leo nyani hana ngozi kwenye makalio aliipoteza siku hiyo. Na hadithi yangu imeishia hapo.

17 February 2013

MPIGA CHABO

Wapiga chabo au peeping toms wako dunia nzima, wengi wamepoteza macho yao Uswahili kwa kuchomwa na misongo, kupuliziwa dawa za mbu au perfume lakini wapo tu wengi bado

16 February 2013

UTOTO RAHA SANAAAAAA


CHILI TOMATO


MTEJA: Nipatie chips mayai
MKAANGA CHIPS: Niweke tomato?
MTEJA: Chili tomato. ….Mkaanga chips akatengeneza chips mayai safi na kuweka chilli na tomato nyingi akampelekea mteja
MTEJA: Chacha hiki nini njomba? Nimekwambia chili tomato we umeweka chili nyingi na tomato nyingi, kama chio chalau ni nini njomba?. Chacha kula wewe mimi nletee nyingine ukiweka tomato mimi chili


15 February 2013

CHUPI YETU

MUME: Unajua mi nakushangaa sana, kila siku nakusikia mara usema TV yangu, gari yangu, chumbani kwangu, watoto wangu, sisi ni wanandoa kila kitu ni chetu, jirekebishe bwana
.........Mke akawa anaendelea na shughuli aliyokuwa kiifanya bila hata kumjibu mumewe......
MUME: Halafu unadharau sana hata husemi kitu, sasa hapo unatafuta nini?
MKE: Chupi yetu

MATOKEO YA VALENTINE DAY 2013


Taarifa fupi kutoka nchi nzima, kuhusu siku ya jana ambazo mpaka sasa zimetufikia kwenye chumba chetu cha habari;
i.                Waume waliofumaniwa..152
ii.              Walioachana…200
iii.             Mauzo ya kinga…..1,267,000
iv.             Wake waliofumaniwa......67
v.              Mauzo ya chips yalipanda kwa aslimia 200
vi.             Mapato ya guest yalipanda kwa asilimia 500
vii.           Wake waliopigwa..... 700
viii.          Waume waliopigwa..... 98
ix.             Wasichana walipigania wavulana.... 298
x.              Wavulana waliopigania wasichana...... 78
xi.             Waliolazwa kwa presha ya kuwakosa wenzi wao kwenye simu... 123
xii.           Mapenzi mapya..... 2000
Tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kadri tutakavyozipata

13 February 2013

MAOMBI MKANGANYIKO

MUME: E Mungu niondoe katika huu umasikini, nifungue katika kifungo hiki cha kukosa fedha, sikiliza kilio changu E Mungu
MKE: E Mungu nisikiliza mimi, usimpe huyu utajiri, atanunua magari ataanza kulewa, atakuwa anasindikizana na wale wasanii mi ataniacha, tuachie huu huu umasikini Mungu

12 February 2013

HAFUNGWI MTU HATA IWEJE


'AI WEWEE, HUYO NI MIMI ZAMANI'

Jamaa kapata mupenzi club, wakaishia kuondoka wote kwenda kwenye nyumba ya mdada. Jamaa kalala vizuri na kuamka kesho yake saa sita, akaoga na wakati anakunywa chai akaona picha kubwa ya mkaka kwenye ukuta;
JAMAA: Sweety huyo ndiye mwenye nyumba nini?
MDADA: Aii wewe, angalia vizuri huyo si mimi zamani...jamaa akapaliwa na mkate

BABAKO ANA HELA?

BINTI: Baba nimepeta mchumba, kijana mtaratibu mcheshi
BABA(Tajiri): Mchumba mwenyewe ana hela lakini?
BINTI: Nyie wanaume wote mko sawa, hata yeye siku ya kwanza tu aliniuliza kama wewe una hela

LEG-LINE YA SUPASTAA WA BONGO 12


ZUNGUMZA KIINGEREZA FASAHA BAADA YA NUSU SAA TU


10 February 2013

LEG-LINE YA SUPASTAA WA BONGO 9


SOMA KITIME 29: 1-5


1. Na ikatokea katika zama za utawala wa awamu ya 4, mara baada ya lile apizo la kuingia katika dijitali, muda mfupi baada ya watu wa kule mbali kuamua kutimiza yale yaliyosemwa toka kale za mababu zao, kuwa kila mtu atapumua kwa gesi yake, hapo ndipo binadamu  wale, wake kwa waume, wakatokewa na matatizo makubwa na kuwa watu wa kutoa visingizio, wengine walisema, chaja yangu iligoma, na wanawali walilalamika kuwa wanaume wa wakati ule hawakutaka kupokea simu zao, wengine walilalamika kuwa imani yao iliwazuia wasiwasiliane na wanawali, na wengine walitangaza kuwa wangechukua muda ule kujifungia ndani na familia zao kwani wanao hawakuwajua wote. Wengine walilalamika kuwa wakubwa zao wa kazi waliwatuma mbali, wengine walidai mama zao wanaumwa katika vijiji vilivyo mbali, wengine walidai kuwa mashine za ATM zilimeza kadi zao, wengine walidai magari yao yaliharibika, wengine wakadai kuwa imani zao ziko katika msimu wa kufunga na kujitafakari na hivyo si vema kufanya sherehe wala hata kucheka. Wengine walidai wamo katika kazi za kuumbua mafisadi na wangezunguka utawala wote kuhubiri ujio wa zama bila ufisadi. Naam naam nawambieni Enyi wanadamu mkiona ishara hizi, msifadhaike, bali shangilieni kwani zinashiria kuwa tarehe 14 ya Februari ikaribu  Kitime 29:1

8 February 2013

ATAKAECHEKA TANGAZO LETU LA KIDIJITALI NI MSALITI

Kikubwa usafiri au vipi? Najua wengine mtaanza kuseeeema, oh sijui nini mbona wale wanatangazo kwenye TV, we unataka tangazo au unataka kufika kijijini kwenu? Hata mbuyu ulianza kama mchicha umeonaeee

LEG- LINE YA SUPASTAA WA BONGO 8


LEG-LINE YA SUPASTAA WA BONGO 7


LEG-LINE YA SUPA STAA WA BONGO 6


MKIPATA HIYO DAWA NIPENI NIMPE NA BABA YAKE

MAMA: He mwalimu hujambo?
MWALIMU: Sijambo Mama Devi, tena bahati tumekutana ilikuwa tukutafute tuongee kuhusu Devi
MAMA: Nini tena huyu mtoto?
MWALIMU: Devi ana akili sana, lakini tatizo lake anapenda sana kuchokoza na kucheza na wasichana, hivyo waalimu tumeona tujaribu kutafuta dawa tumkomeshe hiyo tabia
MAMA: Yaani mwalimu mkipata hiyo dawa ntaiomba nimtibu baba yake, naye yuko hivyohivyo

MAPENZI YETU YAWE SIRIAZ

MDADA: Mpenzi wangu mbona huwa hutabasamu hata kidogo ukiwa na mimi?
MKAKA: Jamani si we mwenyewe ulisema unataka tuwe siriaz kwenye mapenzi yetu? Nikaona nikichekacheka utaniacha

UNAONGEAJE NA NYANI WENGINE NA MIE NIKO?

Jana nilienda kwenye muziki hoteli fulani mitaa ya Sinza, nikabana pembeni jirani na wapenzi wawili walioonekana kuwa wako deep. Ghafla jamaa akaondoka kama anaenda chooni, lakini akapiga kona kali na kutoka nje ya hoteli. Binti nikamuona kabisa hana raha maana aliona ile muv. Baada ya dakika chache jamaa akarudi kwenye meza yake, ile kufika tu binti akaja juu;
BINTI: Yaani unaenda nje kuongea na nyani wengine wakati mi niko hapa.....kidogo nipaliwe na kinywaji changu nikaona niondoke nisije nikacheka nikaonekana mkorofi

7 February 2013

MUNGU NIJALIE KAZI NIJAZE NA MADEMU KWENYE GARI LANGU

Jamaa kamuomba Mungu....Ee Mungu nijalie kazi niwe na mifuko imejaa hela kila siku, gari limejaa mademu kibao, niwe nikifungua mdomo watu wananisikiliza...wiki moja baadae jamaa akapata kazi ya ukonda kwenye daladala

BLACBERRY YAKO SAMSUNG AU NOKIA?

DAVINA: Mambo Sandra, mwenzio nimenunua bonge ya simu
SANDRA: Simu gani? Itakuwa Mchina maana wewe unapenda vya urahisi
DAVINA: A wapi nina Blackberry
SANDRA : Hongera, Blackberry yako Samsung au Nokia
DAVINA: Unanionaje? Kitu Erricson  hiki bibie

LEG-LINE YA SUPA STAA BONGO 5


6 February 2013

HAWATAKI NYAMA YA MBWA MI NIFANYEJE?

Mjamaa alikwenda mji mmoja jina kapuni kumtembelea rafiki yake, chakula kikaja, akajikuta kapewa ugali na nyama nyingi na mwenyeji wake pia akapewa ugali na nyama nyingi, watoto na mke wakawa pembeni wanakula ugali na mboga za majani. Jamaa lika mtach lakini akanyamaza akapanga wakimaliza kula amuulize rafiki yake kwa nini anafanya uchoyo huu. Walipomaliza sahani zimekwisha tolewa na baada ya kunywa maji baridiiiiiii;
JAMAA: Aise sijapenda hii tabia, sisi tumekula ugali na nyama kibao mkeo na watoto wamekula mboga za majani bila hata kipande cha nyama
MWENYEJI:Mi sio kosa langu, wao wenyewe hawataki kabisa kula nyama ya mbwa

LEG-LINE YA SUPA STAR WA BONGO 4


GULO UMEMALIZA UGALI NA MAHARAGE YOTE

MKAKA: Hi uwapi swity?
MDADA: Niko home
MKAKA: Unafanya nini?
MDADA: Nakula
MKAKA: Unakula nini?
MDADA: Mama katengeneza macaroni, ambayo kanyunyizia chiizi na  sausage fulani imported ambazo baba amenunua supermaketi Masaki, na saladi, kisha ntateremsha na Epo juisi, ghafla ikasikika sauti ya mama yake
MAMA: Hivi we Gulo kaka yako atakula nini na we umemaliza ugali na maharage yote?

KASHESHE ZA MESEJI ZA SIMU


Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;
Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
Simu  2- He Mama Joji unaumwa?
Simu 3- Nami pia daima
Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe
Simu 8-Chukua taim yako
Simu 9-?!?
Simu  10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?
Simu 11 – Hivi naota?
Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi mkubwa
Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi

LEG-LINE YA SUPASTA WA BONGO 3


HATA KWETU WAPO


4 February 2013

LEG-LINE YA SUPERSTAR WA BONGO 2


LEG-LINE YA SUPERSTAR WA BONGO


VICHEKESHO YA KENYA
1. Guy:Mwisho wa gari ni wapi?
           Conda:Penye unaona number plate.

2. Konda: Huna pesa ndogo boss.
                                 Passenger: Ikunje mara mbili uone ikikua ndogo.

NYANI DREVA WA GARI LILILOPATA AJALI


Trafiki kakuta bonge ya ajali, dereva na pasenja mwanamke wamefariki. Wakati akiangalia angalia kakajitokeza kanyani, toka uvunguni mwa gari kakawa kana ruka ruka. Trafiki akasema, ‘Ungekuwa unajua kuongea si ungetuhadithia ilikuwaje’ Nyani akatikisika kichwa kuonyesha kaelewa. Trafiki akauliza, ‘Ilikuwaje?’.  Nyani akaokota kopo la bia na kuonyesha ishara ya kunywa, polisi akasema ‘ Walikuwa wanakunywa?’ Nyani katikisa kichwa kukubali. Halafu nyani akaonyesha ishara ya kuvuta sigara, askari akauliza, ‘Walikuwa wanavuta bangi?’  Nyani akatikisa kichwa kukubali, Polisi akauliza ‘Na nini kingine?’ Nyani akaonyesha ishara kuwa walikuwa wanabusiana, ‘ He walikuwa wanabusiana pia?’  Nyani kakubali. Polisi akauliza, ‘Sasa wakati wanakunywa pombe, wanavuta bangi, na kubusiana we ulikuwa wapi?’ Nyani akaonyesha ishara kuwa yeye ndiye alikuwa anaeendesha gari.

2 February 2013

NYOTA ZENU...usiachike bure soma nyota zako

Kwa kweli huwa sipendi sana kutumia utaalamu wangu wa nyota lakini kwa maombi ya wengi nimelazimu kuchukua nafadsi hii kutabili mambo muhimu katika kipindi cha wiki mbili zijazo
Kuanzia leo tarehe 2 February hadi 15 Februari ni kipindi kibaya kwa wapendanao. Kuna wadada wengi watajikuta wanaachika bila sababu maalumu, kitendo cha kumtania umpendae kitaishia kufukuzwa kwa hasira kuu, hii ni kutokana na nyota kuingiliana njia. Bahati nzuri ni rahisi sana kukwepa balaa hili la kuachika. Wadada ni muhimu nasema ni muhimu, kuanzia leo, usitamke neno VALENTINE. Kwa kuwa kinyota neno hilo limezingirwa na nyota nyeusi isiyotabilika na hivyo kuweza kumfanya mpenzi wako asitabirike na kukufukuza bila sababu. Epuka narudia tena epuka kutamka neno VALENTINE na hasa ukuwa umeunganisha katika sentensi moja neno ZAWADI. Balaa hili litapita tarehe 15 asubuhi, hapo unaweza kutamka neno hilo bila balaa yoyote. Ila kwa wale wataakaoachika wasipaniki maana nyota zinaonyesha mambo yatarudi katika hali yake kuanzia hiyo tarehe 15.

WALE WASUPA NANIHII STAIL INGINE HII HAPA


UJUMBE KWA WACHORA KATUNI aka MAKAVU LAIVU YAO

Halo, tafadhali ujumbe huu unawahusu wachora katuni aka wachora vibonzo. Hebu simameni kwanza niwaone wote. Masoud, Marco aka Ka-kobe, Aloys, Kakakeri, Twalipo, Katembo, mLevy, Nko, okay, wengine wako wapi?,King Kinya yuko wapi? ohh kwenye GESI? (Nimesema gesi siyo gesti, msinianzishie bifu na best wangu)
Poa. Sasa hivi nyie watu mnajua matatizo ambayo mnaniletea? Hivi mnaona ni sawa kabisa kuweka vibonzo ambavyo vinasababisha mi niwe nacheka hovyo kwenye vihais kama mwehu? Why men? Mtu unakuwa na akili gani kufikiria kibonzo eti mtu akichanganya mno vyakula ataota kaolewa, je hiyo ndio sera inayoweza kuleta maendeleo kwa sisi vijana wa kizazi hiki? Kwanini hamchori mambo ya kimaendeleo kama mashamba ya Ujamaa na kujitegemea au usafi wa Kinondoni au kilimo cha kufa na kupona au gesi…..ehhh hapana msichole gesi itakuwa soooo, yaani choleni mambo ya maana, ili niweze kujizuia kununua magalizeti mengi kwa mpigo ili nisikose mipicha yenu ya ajabu ajabu. Kumbukeni vitabu vya wahenga vilisema CHEKESHENI NANYI MTACHEKWA, ohoooo nyie haya. Kuanzia kesho mkinichekesha naenda kuchoma moto nyumba za wabunge wenu.

1 February 2013

CHEKA KIDOGO


Du mie sina sumu

DEVI: Aise nimekuwa namkutafuta siku nzima
FULO: Kwani vipi?
DEVI: Ndugu yangu nina matatizo lazima ikifikia saa kumi na mbili niwe nimepata milioni 3 au italazimika ninywe sumu
FULO: Duh pole maana mimi sina sumu mshkaji

MAPENZI HAYACHAGUI SURA


KIJANA WAKO WA KAZI KAFA!!!!!

Baada ya mkewe kujifungua mtoto, jamaa akafurahi sana lakini baada ya muda mfupi furaha yake ikaanza kupungua alipoona mkewew muda mwingi anashughulika na kabebi, si akaanza kukaonea wivu kabebi, akaamua kumaliza ugomvi akamtaim mkewew alipolala akapaka sumu kwenye chuchu za mkewe. Asubuhi akaondoka kwenda kazini akijua akirudi atakuta kabebi kamekufa. Na kweli haukupita muda jirani yake akampigia simu,
JIRANI: Mheshimiwa rudi nyumbani kuna msiba
JAMAA: Masikini mwanangu kafa, masikini mtoto wangu
JIRANI: Hee kwanini unasema hivyo? Mtoto wako na mama yake wako salama salimini, aliyefariki hi huyu kijana wako wa kazi