HATUPIMI BANDO

26 January 2013

SWAGA ZA KIJIJINI


Swaga za jamaa yangu aliyekaa Dar kwa muda mfupi sana sasa karudi kijijini;
WAMJINI: Unajua msikaji Ulaya na Tanzania tofauti ndogo sana. Kama sisi huku Tanzania hata kule wana timu mbili tu kubwa, Manjesta na Asno. Hawa Manjesta wamejenga ofisi sao na kiwanja nje kidogo tu ya  Landan, unapanda fidaladala fiwili tu umefika. Aliyeanzisa timu ni kababu fulani  kachawi hako, uchawi wake kanatumia bablish, wakianza kuchesa tu kanaanza kutafuna bablish, kakimesa tu, ujue hapo mmefungwa. Na hawa Asno nao  wako katikati ya jiji, unajua Landan kama vile Daslamu tu hakuna tofauti, kuna Manzese, Magomeni, Yombo, sasa hawa Asno wako Yombo ya Landan, kuna fi Hais unadandia unamwambia tu konda, ‘Msaada Asno’, basi wanakususa kwenye kiwanja chao, na hawa nao timu yao alianzisa babu moja anaitwa Asno Wenga, nako kachawi hako, mwiko wake hakaruhusiwi kucheka, kakicheka tu mjue Asno itafungwa. Nasikia mwaka jusi kalikuja mbaka Samunge kwa Babu wa kikombe, timu ilikuwa inafungwa sana, kalipokunywa tu kikombe wacha timu ije juu.
WAKIJIJINI: Bwana we muongo bwana umejuaje hayo?
WAMJIJI: Si nilikwenda kutembelea mjomba, nikakuta ana TV, ukiminya namba 5 kwenye kidude fulani inatokea DSTV, hapo unapata siri sote za mpira wa Ulaya.
Unajua sisi tungekuwa tunawafwata wale tungefika mbali sana, we ujue wanatumiaga mpaka uchawi wa mvuto, unawasaidia kujaza watu kwenye viwanja vyao, we acha bwana jinywee tu huo ulanzi wazungu we waache bwana

No comments: