HATUPIMI BANDO

28 January 2013

KANICHOKOZA JE NIPIGANE NAE?


Binadamu wakiudhiana mara nyingine huamua kutwangana ngumi. Unapojikuta umeingia katika mtiti wa kutwangana ngumi, akili zako lazima zifanye kazi haraka sana na maamuzi magumu au mepesi lazima yatolewe tena mara nyingine bila kutoa nafasi ya ubongo kufikiri. Lakini je, ungekuwa ubongo wako unafanya kazi kiserikali serikali ingekuwaje?
Kwanza baada kujikuta umeingia katika mtiti wa ngumi ingelazimu Katibu Mkuu husika aite maafisa wake kuona faida na athari za kutwangana ngumi, kisha baada ya kupata jibu hili ungelazimika kufanya maamuzi kama je ujitetee au la, na kuna matatizo gani kisheria ukiamua kujiunga kwenye hizo ngumi. Ungeamua kujitetea ingelazimu uite maafisa wengine kutafiti madhara ya kupigwa hadharani, au je kuna matokeo gani ukimtandika mpinzani wako ngumi ya kushoto, na je ataangukia wapi? Na kama angeakukia jiwe na kichwa kupasuka je matokeo yake  yangekua nini? Na umma ungelichukuliaje hili? Hapo ndipo ripoti nzima ingetolewa na kujadiliwa kuona kama kuna sababu ya kuendelea na ugomvi huo. Shida tu ni kuwa mwenzio asie na urasimu angekuwa kesha kupa mkong’oto wa nguvu

No comments: