HATUPIMI BANDO

30 January 2013

FB STATUS UPDATE

KUNA MDADA NIMEFUATILIA FB STATUS UPDATE KWA MIEZI MIWILI:-
NOV 16, 2012-Wow! THIS IS IT kama alivyosema Michael Jackson, I just found the love of my life nothing will ever stop me from loving my man!, najua mtasema sema sanaaaa haloooooooo
NOV 30 2012- YAANI, wanaume maudhi matupu
DEC 1 2012 -Never make someone a priority to
you when you are just an option to them!
DEC 4 2012- NIKO SINGO, I am happy to remain single and I
will never fall in love again!
DEC 9 2012- I'm looking for a man to love and
treat me right. Niombeeni my friends
DEC 24 2012-When you deeply fall in love with a
person, you realize why it didn't work with anybody
else but him. I love my guy so much. mwaaah!''
JAN 3 2013- All men are the same, ni wanyama believe me

WAPOGORO NAO WAINGIA KATIKA MFUMU WA DIJITALI

Na Wapogoro nao waokumbukwa na NOKIA;
Phonebook-Shitabu sha simu
Names- Matawa
Exit- Kulawa
Cancell- Kudumula
Settings- Kunyawa
Games- Mishinigu
Call- Mshemu
Missed Call- Mshemu gudumukira
Received calls- Mshemu Gwankiti
Diaaled Calls- Mshemu Gugombiti
Messages- Ujumbi
Vibration- Kulindima
Na ukimpigia mtu asie hewani unataarifiwa na mdada,'Namba ya muntu yugumgombera ipatikana ndiri vinu, shondi shondi,gumgomberi kai shirau' Habari ndio hiyo, maswaliiiiii?

28 January 2013

KANICHOKOZA JE NIPIGANE NAE?


Binadamu wakiudhiana mara nyingine huamua kutwangana ngumi. Unapojikuta umeingia katika mtiti wa kutwangana ngumi, akili zako lazima zifanye kazi haraka sana na maamuzi magumu au mepesi lazima yatolewe tena mara nyingine bila kutoa nafasi ya ubongo kufikiri. Lakini je, ungekuwa ubongo wako unafanya kazi kiserikali serikali ingekuwaje?
Kwanza baada kujikuta umeingia katika mtiti wa ngumi ingelazimu Katibu Mkuu husika aite maafisa wake kuona faida na athari za kutwangana ngumi, kisha baada ya kupata jibu hili ungelazimika kufanya maamuzi kama je ujitetee au la, na kuna matatizo gani kisheria ukiamua kujiunga kwenye hizo ngumi. Ungeamua kujitetea ingelazimu uite maafisa wengine kutafiti madhara ya kupigwa hadharani, au je kuna matokeo gani ukimtandika mpinzani wako ngumi ya kushoto, na je ataangukia wapi? Na kama angeakukia jiwe na kichwa kupasuka je matokeo yake  yangekua nini? Na umma ungelichukuliaje hili? Hapo ndipo ripoti nzima ingetolewa na kujadiliwa kuona kama kuna sababu ya kuendelea na ugomvi huo. Shida tu ni kuwa mwenzio asie na urasimu angekuwa kesha kupa mkong’oto wa nguvu

26 January 2013

KINYOZIIIIIIIII


MKE WANGU ANATAKA KUJIRUSHA DIRISHANI

Mtu na mkewe walipanga chumba juu katika hoteli ghorofa ya 10. Mume akampigia simu meneja;
MUME: Hall meneja, hebu njoo huku chumbani kwetu, mi na mke wangu tunagombana na mke wangu anatishia kuwa atajirusha kwenye dirisha
MENEJA: Hayo ni mambo binafsi mi siwezi kuingilia
MUME: Hapana jambo hili linakuhusu sana, huku dirisha halifunguki, njoo utengeneze

MKEO TULISHAWAHI WOTE

MUME: Aise tafadhali salimiana na mke wangu Fulo
JONI: Dah kumbe huyu ndie mkeo, namfahamu sana
MUME: He umemfahamia wapi tena jamani?
JONI: Fulo na mimi tulishwahi kulala wote si tukakamatwa
MUME: Umesema nini we mshenzi?
JONI: Tulikuwa darasa moja praimari, tukalala usingizi darasani wakati mwalimu anafundisha,akatukamata, tulikula mboko za nguvu.

PEDESHE KAKUPINDUA

Mke kaamka analia;
MUME: Jamani vipi tena mbona unalia asubuhi hii?
MKE: Nimeota Pedesha mmoja, bonge ya hendsam, kaja kakupiga sana, halafu akanichukua nikawa mke wake
MUME: Hahahahaha, hiyo ni ndoto tu mke wangu
MKE: Ndio maana nalia

SWAGA ZA KIJIJINI


Swaga za jamaa yangu aliyekaa Dar kwa muda mfupi sana sasa karudi kijijini;
WAMJINI: Unajua msikaji Ulaya na Tanzania tofauti ndogo sana. Kama sisi huku Tanzania hata kule wana timu mbili tu kubwa, Manjesta na Asno. Hawa Manjesta wamejenga ofisi sao na kiwanja nje kidogo tu ya  Landan, unapanda fidaladala fiwili tu umefika. Aliyeanzisa timu ni kababu fulani  kachawi hako, uchawi wake kanatumia bablish, wakianza kuchesa tu kanaanza kutafuna bablish, kakimesa tu, ujue hapo mmefungwa. Na hawa Asno nao  wako katikati ya jiji, unajua Landan kama vile Daslamu tu hakuna tofauti, kuna Manzese, Magomeni, Yombo, sasa hawa Asno wako Yombo ya Landan, kuna fi Hais unadandia unamwambia tu konda, ‘Msaada Asno’, basi wanakususa kwenye kiwanja chao, na hawa nao timu yao alianzisa babu moja anaitwa Asno Wenga, nako kachawi hako, mwiko wake hakaruhusiwi kucheka, kakicheka tu mjue Asno itafungwa. Nasikia mwaka jusi kalikuja mbaka Samunge kwa Babu wa kikombe, timu ilikuwa inafungwa sana, kalipokunywa tu kikombe wacha timu ije juu.
WAKIJIJINI: Bwana we muongo bwana umejuaje hayo?
WAMJIJI: Si nilikwenda kutembelea mjomba, nikakuta ana TV, ukiminya namba 5 kwenye kidude fulani inatokea DSTV, hapo unapata siri sote za mpira wa Ulaya.
Unajua sisi tungekuwa tunawafwata wale tungefika mbali sana, we ujue wanatumiaga mpaka uchawi wa mvuto, unawasaidia kujaza watu kwenye viwanja vyao, we acha bwana jinywee tu huo ulanzi wazungu we waache bwana

24 January 2013

SWAGA ZA WADADA


SWAGA ZA WADADA ZETU ILI WAONEKANE NAO WAMO HASA WAKITOKA USWAZI WAKAWA WAMENDA OUT MITAA YA USHUANI;;;
1. Halima………muhudumu naomba unilete salad ya moto, na chupa ya Amarula.
2. Chausiku…..nipe PIN yako niwe nakupigia
3. Siwema….nimechokaje, nimeshinda Shoprite  natengeneza nywele
4. Gulo….Boifrend wangu kanambia likizo ya  summer mwaka huu London nikale Chrismas
5. Cynthia…Nimenunua  BlackBerry wamenambia PIN nikaipitie kesho
6. Fulo....Mi napendaga kusafiri na Presishen, napenda viti vya dirishani, mtu unakaa unafungua kioo chako hewa safiii mpaka mwisho wa safari.
7. Fatu….kiukweli mi niliipenda London kuliko Uk

MPENZI WANGU TOKA UVUNGUNI

Jamaa karudi home ghafla na kupata mshtuko kukuta mkewe mpenzi ana bwana ndani, baada ya zogo kubwa, wanaume wakaenda ukumbini kumalizana kiungwana;
MUME: Sikiliza mi nakusamehe niachie mke wangu ananipenda ila ni shetani tu kampitia
MGONI: Lakini mimi niko nae siku nyingi, hawezi kuniacha ananipenda sana
MUME: Hebu tufyatue risasi na kujifanya tumeuwana atakayeliliwa zaidi achukue mke....wakafyatua risasi mke akaja mbio akipiga kelele na kukuta wanaume wamelala chini......akaanza kucheka na kurudi chumbani
MKE: Mpenzi wangu toka huko uvunguni wale mafala wamejipiga risasi wamekufa wote

23 January 2013

JE UMESHAPATA UGONJWA WA FACEBOOKMANIA? ANGALIA MATOKEO YAKE(VIDEO)

                 JE UNAKICHAA CHA FACEBOOK?

ALAMA KUWA UMELOGWA


Kwa bahati mbaya kuna Wabongo wana roho mbaya, na mbaya zaidi wanaweza kukuendea kwa mganga hata kijijini kwao ili tu usifanikiwe. Lakini pia kuna ndugu huko kijijini kwenu ukienda kuwatembelea linakuwa kosa, wanaamua kukupiga kitu mambo yako hapa mjini yanakwama kishenzi. Nimekusanya hapa baadhi ya mambo ambayo ukiona tu yameanza kukuandama ujue kijijini kwenu wamekuendea kwa mganga;
i.                Ukiona kila unapodownload kitu ikifikia  99% hakiendelei ujue tayari
ii.              Ukiona umenunua Blackberry kwa shilingi laki 7, kesho yake unakuta duka jingine wanauza ileile kwa shilingi laki 3 na nusu ujue wameshakushughulikia
iii.             Ukiona hata ukitumia pafyumu gani, kikwapa kiko palepale ujue tayari
iv.             Ukiona watu wote wanatanua, na wewe ukafuata ukajikuta unakamatwa peke yako ujue wameshafanya mambo kijijini kwenu
v.              Unaingia chumba cha intaview unajikuta umesahau hata jina lako, hapo ujue tayari
vi.             Ukikosea ukajikuta umetumia super glue badala ya matone ya dawa ya macho, hapo wameshakutwanga
vii.           Unakuta mchwa wamekula jina lako tu kwenye vyeti vyako vya shule we nione jamaa wameshakuchapa

DREVA SIMAMISHA

Mlevi alipanda daladala akiwa anatoka Msasani anaelekea kwake Ubungo, mara simu ya mdada jirani yake ikalia;
MDADA: Hellow, Sweety mambo? Niko kwenye daladala naelekea Kiwalani kwa shangazi kuna msiba ntakutafuta nikifika. Baada ya muda simu ya mtu mwingine ikalia;
JAMAA: Hello, aise nivumilie hapa niko kwenye basi naelekea Ifakara nikirudi ntakupa mzigo wako. Simu ya konda ikalia,
KONDA: Vipi mshikaji, leo noma mwanangu, nimepata zali hapa napiga mzigo niko daladala la Mwenge Kunduchi.
MLEVI: Dreva simamisha gari nataka kushuka maana sijui hili gari linelekea wapi

22 January 2013

JOTO BAYA


KAOGEEEEEEEE

Ukiwashwa kiganja wanasema utapata pesa, ukiwashwa jicho wanasema kuna mtu anakuteta. Ukiwashwa sehemu za siri ujue hizo fungus..kaogeeeeeeeeeeee

17 January 2013

HELOO HAPO MIREMBE?

JAMAA: Hapo Mirembe?
NESI: Ndio
JAMAA: Hivi chumba na 17 kuna mtu?
NESI: Ngoja niangalie...ahh hakina mtu vipi?
JAMAA: Niliona nipige simu nicheki kama kweli nimetoroka au bado

WHERE DID YOU WENT?


Nimekuwa nazunguka sehemu nyingi hapa Dar kupata vituko, lakini kwa kweli hizi sehemu wanazokwenda enjoy wale wanaojiona  wako juu kuna vituko vikali sana, kwa kawaida huwa nakaa pembeni na Fanta yangu nasikiliza vituko, sasa kuna hawa wakaka na wadada ambao hutaka kuongea Kiingereza tu kusudi kuonekana wao wako kidijitali zaidi, yaani we acha tu. Ukitaka upate utamu huu live nenda kwenye bar zote karibu na vyuo hasa baada ya wanachuo kupata mshiko wao, wenyewe wanauita BOOM, nenda club  za Masaki, nenda Samaki samaki na sehemu kama hizo, utasikia kiingereza kifuatacho;
i.              Where did you went?
ii.           I come to your office yesterday but I didn't find you.
iii.         Where is the second leg of my shoe?
iv.         I enjoyed the movie, it is very interested
v.            God bless you with a children
vi.         "She dided it"
vii.       I will better kill myself than commit suicide.
viii.    Can you hear the smell?
ix.         Arsenal and Man U are the greater rivalry in England.
x.            I was come
xi.         We are mucher than them
xii.       Remember me to give you your money tomorrow
xiii.    This film is very sweet

Guys if this is how you people speak english, include me out.

16 January 2013

HILOOO SIO ISHU SWITYY

Jamaa alikuwa kwenye Hummer na mbebs wa ukweli, ambaye wakati huo alikuwa akilamba ice-cream huku kiyoyozi kinampuliza, gari liko kwenye silence;
MJAMAA: Bebi kuna kitu nataka kukwambia lakini najua utaniacha
MBEBS: Sema tu swity
MJAMAA: Usikasirike lakini mpenzi
MBEBS: We sema tu hanii
MJAMAA: Nimekuficha muda mrefu lakini, kiukweli mi nina wake wawili
MBEBS:Hahahahahahahaha hilo tu swity nilidhani unataka kusema gari hili sio lako

BOSI WETU BABA MKWE WANGU

Baada ya mke kupokea kipigo kikali toka kwa mumewe, akakimbilia police post.
MKE: Mume wangu anauza madawa ya kulevya, alivyoona nimemgundua kanipiga sana.....POLISI WAKAMFUATA MUME WAKAMUARESTI NA KUANZA KUMPA KIPIGO CHA MBWA MWIZI AELEZE WAPI ALIPOFICHA MADAWA. HATIMAE JAMAA AKAKUBALI KUSEMA;
MUME: Wacha niseme ukweli, mimi nilitumwa tu na bosi wetu, na mzigo anao yeye.
POLISI: Bosi wako ni nani
MUME: Bosi wetu ni baba mkwe wangu

15 January 2013

DENDAAAAAA


TUMWAMBIE MUMEO AU?

Jamaa kenda kwa Mwenyekiti wa serikali za mtaa,
JAMAA: Mke wangu hataki kunipa unyumba hebu ongea nae, nimekuja nae.
MJUMBE: Hebu muite, we kaa nje ya ofisi niweze kumsikiliza
JAMAA: Poa mkuu
MJUMBE: Haya mama kunani tena huko mzee unamnyima unyumba?
MKE: Asubuhi naondoka nyumbani sina senti tano nachukua kibajaji mpaka kazini nikimwambia dreva sina hela, ananiuliza sasa utanilipa badae au? Mi nakubali au. Nakuwa hapo nimechelewa kazini, nikifika huko bosi anasema sasa umechelewa nikufukuze kazi au? Mi nachagua au, jioni narudi nyumbani tena mwenye kibajaji ananiuliza unalipa au? nakubali au, sasa nakuwa nimechoka mzee akitaka namnyima.
MJUMBE; Dah hiyo stori ya kusikitisha, sasa tumwambie mumeo au?

JOKATE ULITAKIWA UPATE KIBALI CHA SERIKALI

Kwa kweli mimi na Watanzania wenzangu tumepata mshtuko mkubwa baada ya kusoma habari hii. Mpaka sasa tunajiuliza Why Jokate Why?. Wewe unaelewa taratibu kuwa mtu anapotaka kuchumbiwa huwa haifanywi siri, jambo la kwanza unaenda kwa Afisa Utamaduni kuomba kibali, ambacho unatakiwa kukipitisha vituo vya polisi vya jirani kisha kibali hicho kupigwa muhuri na Katibu Mtendaji wa kata unayotegemewa kuchumbiwa, na hatimae kupitia kwangu afisa Vibali vya Kuchumbiwa, ambapo huita Press Conference kutangaza uchumba. Hizi ni taratibu tu za kawaida za kiutendaji kiserikali, sasa wewe umezikiuka, isingekuwa ujasiri wa waandishi wetu makini tusingejua ungekuwa umevunja sheria na 6 ya 1956 ya Uchumbalization Act. Therefore next time fuata taratibu au mfwate mwandishi ili akuelekeze taratibu ili uchumbiwe kwa vibali vinavyotakiwa.
Afisa Vibali vya Uchumba

14 January 2013

SERIKALI ICHUNGUZE SPONJI ILIYOWEKWA KWENYE VITI VYA BODABODA

-->
Honda 90
Pikipiki ya kwanza
Pikipiki zilianza kutumika Ujerumani katika karne ya 19. Ulikuwa usafiri uliokuwa mpya lakini ulirahisisha usafiri hasa ukukimbuka watu wa huko wakati huo wengi walitumia wanyama kwa usafiri. Huku kwetu enzi ya Muingereza ndio pikipiki zilianza kusambaa sana na kati ya pikipiki zilizopendwa zilikuwa za aina ya BSA kutoka Uingereza, pikipiki hizi zilipata jina kutoka kampuni iliyokuwa inazitengeneza iliyoitwa Birmingham Small Arms company. Baada ya Uhuru pikipiki za Honda na Suzuki kutoka Japan,  zilikuwa maarufu sana hapa nchini, kwani kuna wakati serikali iliwapatia Makatibu Tarafa , Mabwana Shamba na watumishi wengi wa serikali pikipiki aina ya Honda 90 na baadae Honda 125. Miaka yote hiyo waendesha pikipiki walikuwa watu wastaarabu walioheshimika na kuheshimu sheria za barabarani. Miaka hii michache zimeingia pikipiki za Kichina, ambazo zimezagaa kwenye biashara inayoitwa Bodaboda. Waendesha bodaboda wamekuwa watu wa ajabu ambao hudhani kuwa wao wana haki ya barabara na hata pembeni ya barabara kuliko mtu mwingine yoyote, na kuwa wao sheria za barabara haziwahusu. Pia ni watu wanaoamini kuwa ukipiga honi tu inatosha hata miti inahama wakati wao wakitaka kupita, mamia wanajeruhiwa na wengine kufa kwa ajaili za kila siku za usafiri huu. Naomba serikali ifanye uchunguzi kwanini watu wakiendesha hizi pikipiki za Kichina akili inahama? Mimi na mashaka na sponji inayotumiwa kwenye viti vya Bodaboda, inawezekana ina madini ambayo yakimuingia anaeiendesha akili inahama. Serikali ifanye uchunguzi wa wasiwasi wangu huu. Kwa kuwa sioni sababu kwanini waendeshaji wa zamani walikuwa hawapotezi akili. NAWASILISHA HOJA

CHANGANYIKIWA


Mihanyenye, NOKIA wameboresha huduma kwa kuweka Kigogo kwenye simu zake


Phonebook-CITABU CE CIMU
Names-MATAGWA
Time-MAPANGO
Ringtones-MILILO
Settings-KUBIDULA
Call-TOWEE
Missed calls-WONO WAKUKULONDOLA
Received calls-WONO WAKUTOWELA
Dialled calls- WONO KUWATOWELA
Games-MIDAWALO
Menu- CITANJILO
Vibration-MCICIMO
Leteni mihela niwauzie hizo simu

NOKIA YABORESHA SIMU YAJA NA YA KIBENA

NOKIA yaboresha mambo kwa WABENA, simu zawa na MENU ya Kibena
PHONE BOOK-Hitabu sha matawa
NAMES- Matawa,
TIME-Umuda
RINGTONES- Mililo
SETTINGS-Imipangililo
CALL-Tove
MISSED CALLS- Isimu dze hali dzitovilwe
RECEIVED CALLS-Isimu idzanuhilwe
DIALLED CALLS- Dze handile witova pa mwandi
GAMES- Imikino
MENU-Ihivangilo sha hwanza
VIBRATION- Imitetemo

BREAKING NEWS... NOKIA WALETA SIMU KWA KISUKUMA

Baada ya kuja simu za makabila kadhaa sasa ni simu yenye lugha ya Kisukuma;
Phonebook-Shitabo sha simu
Names- Mina
Time- Makanza
Ringtones- Mililo
Settings-Mabhegejo
Calls-Lila
Missed Calls- Lila njimeji
Received Calls-Lila mbokelwa
Dialled calls-Lila ntulwa
Game-Ligusha
Menu-Agalemo
Vibration- Ndetemo
Bhvaveja

Meseji nyingine zina weza kukuharibia wiki

Text zinazoweza kuharibu pozi:
1) Nina mimba yako
2) Sikutaki tena
3) Samahani nimepata ajali na gari lako
4) Nimemuona shemeji anaingia gest na mtu, ntakutumia picha
5) Nimepima majibu sio mazuri, mi najiua
6) Tafadhali muache mume/mke wangu onyo la mwisho
7) Nakuja kuchukua hela zangu

9 January 2013

BREAKING NEWSSSS--MZIGO TOKA CHINA UMEINGIA

Wahini kutoa oda mzigo ndio umeingia jana, na si mkubwa sana, bei maelewano

MKEO HAJUI KISWAHILI

MLEVI 1:Niambie ukweli , wewe ni kama ndugu yangu, hivi kwani watu mtaa huu wanamfwatafwata sana mke wangu?
MLEVI 2: Unasikia bradha mi ntakwambia ukweli. Mkeo ana matatizo hajui kiswahili sawasawa
MLEVI 1: Toka lini? Mke wangu anajua kiswahili vizuri sana
MLEVI 2: Kwa kweli bradha mke wako anajua maneno mengine ya kiswahili lakini hajuo neno hapana

KATI YA MIMI NA MAMA YAKO UNAMPENDA NANI ZAIDI?

BABA: Kati ya mimi na mama yako unampenda nani zaidi?
DOGO: Nawapenda wote
BABA: Mimi ningeenda Dubai halafu mamako akaenda London, we ungeenda wapi?
DOGO: Ningeenda London
BABA: Kwanini?
DOGO: London nakupenda
BABA: Je, mi ningeenda London mama yako Dubai we ungeenda wapi?
DOGO: Ningeenda Dubai
BABA: Hee, unanikwepa unamfwata mama yako
DOGO: Hapana, London si ningekuwa nilishakwenda

8 January 2013

WEZI NCHINI WATANGAZA MGOMO

Hatimae wezi nao wameamua kutumia nguvu za umma kupata haki zao. Wezi wa Tanzania wamepanga kufanya mgomo wa kuiba chochote kuanzia kesho hadi hapo serikali itakapokubali kuongeza siku zao kutoka siku za mwizi kuwa arobain na kuongeza kufikisha themanini. Hii imekuja baada ya kamati kuu ya wezi kuona kiwango hiki kimepitwa sana na wakati ukikumbuka kiwango hiki kilipoanza kutumika, hata ukubwa wa mali iliyokuwa ikiibiwa ilikuwa ndogo sana, na hata kuficha ilikuwa rahisi, wezi waliweza hata kuchimbia chini ya kitanda mali zao na ikawa salama, lakini sasa usumbufu umekuwa mkubwa sana ambapo wezi  hulazimika kuficha mali ya wizi mpaka nchi kama Uswisi umeonaee, siku 40 kwa kweli ni chache sana. Wizi wa zamani ilikuwa mtu unaiba halafu watu wanakufukuza wakikukamata wanakupeleka p[olisi bila kipigo, na ukiwapa mali yao wanakuachia, na mara nyingi ukiwahi kuingia katika chaka wanaogopa kukufuata na tatizo limekuwa linaisha lakini siku hizi, imelazimika kubadili mbinu kwa wananchi hawaoni tabu kukuchoma moto ukijidai unajificha kwenye chaka, hata kwenye nyumba ukiingia wanachoma moto. Katika ule wizi wa kidijitali tayari kuna wanoko wameingilia kati na wanajua mara moja umeficha nchi gani fedha au mali, kwa hiyo ili kuwe na fairplay siku za mwizi ni lazima ziongezeke Mmoja wa wezi ambaye alihudhuria mkutano huo muhimu alisema wazi kuwa Tanzania bila mgomo itakuwa tabu sana ombi lao kupitishwa mapema kutokana na utendaji mbovu wa serikali.

KWA WAGOGO TU

Mihanyenye, 
NOKIA wameboresha huduma kwa kuweka Kigogo kwenye simu zake;
Phonebook-CITABU CE CIMU
Names-MATAGWA
Time-MAPANGO
Ringtones-MILILO
Settings-KUBIDULA
Call-TOWEE
Missed calls-WONO WAKUKULONDOLA
Received calls-WONO WAKUTOWELA
Dialled calls- WONO KUWATOWELA
Games-MIDAWALO
Menu- CITANJILO
Vibration-MCICIMO
Leteni mihela niwauzie hizo simu

TUKAWAMBIE TUMENUNUA MLIMANI CITY

Tukawaambie tumewanunulia Mlimani City au vipi?

MAMBO YA KIDIJITALI


6 January 2013

ILI MSINISAHAU!!!!!!!!!!!!!!!!

Naitwa John Kitime, nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza ‘bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, maana baada ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto wachanga. Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya kuchekesha, kama vile  watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, na kilabuni, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na vyuo mbalimbali nchini na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na huko nilikutana na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua kuchekesha wakijitahidi kuchekesha, cha kushangaza si nikakuta wengine hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho cha kuchekesha wachekaji.
Katika kiota hiki cha www.chekanakitime.blogspot.com , ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.
Pia mimi ni mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui kucheza, hasa Chacha ndio kabisa halafu siku hizi kuna hii inaitwa Kwaito, wakati najitahidi kujifunza imeanza Azonto,  jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio mbadili? Halafu huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?

Daluga za timu ya jamaa zetu


KWELI YULE NI MWANAWE

Mlokole mwenye guest alikataa yanki mmoja aliyekuja na mama mtu mzima kupata chumba akisisitiza kuwa guest yake hairuhusu uasherati. Yule mama akaja juu na kumwambia Mlokole kuwa yule kijana ni mwanae, basi wakapewa chumba. Mlokole akamtuma muhudumu mmoja akachungulie kwenye dirisha la wapangaji hao  ili kuona kama kweli ni mtu na mzazi wake. Baada ya muda muhudumu akarudi na jibu,' Mzee kweli wale ni mtu na mtoto wake, nimemuona yule mama anamnyonyesha mwanae'

NYIE MNAHANGAIKA NA MKOROGO WENZENU WANATAKA KUWA WEUSI


BARUA YA WAZI KWA MHESHIMIWA...naomba uniteue


Mheshimiwa, salamu,
Mheshimiwa mimi ni mwananchi mtanashati, mrefu mnene mwenye mwanya wa wastani, mwenye mwendo wa maringo hatua za hesabu, tabia ya pekee na shingo ya upanga, umeonaee.
 Kwa kweli nimekuwa nasikiliza ushauri wako kuwa wananchi tutengeneze ajira sisi wenyewe, Mheshimiwa mimi nimegundua ajira ambayo itaniletea manufaa na pia kuliletea Taifa letu changa mapato mengi umeonaee. Mheshimiwa naomba uniteuwe wadhifa wa Katibu KATAKATA Mkuu Tanzania. Hadidu rejea za wadhifa huu  ni kuwa mratibu wa Kata kata zote nchini. Labda nitoe maelezo mkuu, hapa nchini kuna watu wanakatakata mambo bila mpangilio, kwa kunipa cheo hicho nitaanza kuratibu katakata zote na hivyo kutoruhusu  mtu kukata kitu bila kupewa stika ya ushuru, na hivyo kila kukata kutalipiwa umeonaee.
 Kimsingi chochote chenye neno KATA ni lazima kipewe kibali na mimi Katibu Kata Mkuu. Ni wazi nitaanza na hawa wanaokatakata umeme, ni lazima wapate kibali ambacho watalipia kodi na ndipo kuruhusiwa kukata. Kuna wengi tu wanaotumia bure huku kukata, kwa mfano hawa wanamuziki wa Njenje wanawimbo wao wanasema, ‘Kata kata , kata chako mwenyewe, kata mwenyewe hayuko’ na hivyo kuhamasisha watu wakate kiuno bure, hii iwe mwisho sasa, watalazimika kupata stika ya kodi kabla ya kuimba wimbo wao huu, na wote wanaokata kiuno walipie ushuru kwa kufanya hivyo.
 Kuna watu wengi tu wana Kata tamaa, bila taarifa yoyote, wengine wana kata kiu bure kabisa bila kulipia kodi, kuna wale wanao kata roho hawamuelezi mtu kwa hiyo kulinyima Taifa letu changa mapato, hii si sawa umeonaee. Mheshimiwa nadhani utaweza kuona ukubwa wa kodi ambayo tutaweza kukusanya ni zaidi hata ya mapato kutokana na madini, hata hawa jamaa wakitaka kukata gesi isije huku, watalazimika kuniomba kibali ili walipie kodi. Hata tukichukulia wale wanao kata kodi, kata tiketi, kata shingo, au hata wale wanao wakata wenzao kilimilimi, au kuwakata ngebe, ni lazima walipie. Hawa wanaotaka kukata kauli ni vyema tukawatengenezea mazingira wawahi kulipa kabla hawachukua uamuzi huo mgumu umeonaee. Nami nitateua makatibu wa katibu katakata, kutoka kata mbalimbali kuratibu katakata zozote ili kusikatike mtiririko wa makato ya wakataji nchini umeonaee
MKUU NOMBA UNITEUE NIWE KATIBU KATAKATA MKUU WA TAIFA nawasilisha hoja.

4 January 2013

HAMSINAKUMI

MWALIMU: Joni 30 +4?
JONI: Thelathini na nne
MWALIMU: Safi sana. Fulo 40 +6?
FULO: Arubaini na sita
MWALIMU: Safi sana. Haya gulo 50+10?
GULO: Hamsinakumi

VIDONGE VYA UMILIONEA

JE UNATAKA KUWA MILIONEA? HATIMAE VIDONGE VIMEGUNDULIKA. NITUMIE SHILINGI ALFU KUMI KWA AJILI YA CHUPA YA KWANZA YA DAWA ZA UTAJIRI

HAYA KACHEZE NIONGEE NA MWENZIO

Lilikuwa dansi la shule mbili za sekondari za bweni, moja ya wadada nyingine ya wakaka. Wadada wawili walikuwa wamekaa peke yao mmoja ana sura mbaya mwingine ana sura nzuri. Yanki mmoja akawaibukia, akamuendea mwenye sura mbaya,
YANKI: Sista unapenda kudance?
MDADA: (Akasimama kwa furaha) Sana tu
YANKI: haya nenda kacheze nataka kuongea na rafiki yako

MAMA ATARUDI SASA HIVI

MDADA: Ujue mama atarudi sasa hivi
MKAKA: Kwani nimekufanya chochote?
MDADA: Ndio maana nakwambia fanya haraka kabla mama hajarudi

MWE MWE MWE KIMPUMU KYA LEO KYAMOTO KWELI NALOLI


TAFADHALI KOJOA HAPA

Jamaa alikuwa kisha choka na watu waliokuwa wanakuja kukojoa kwenye kichochoro nje ya dirisha lake. Hata alipoweka matangazo kama, Usikojoe hapa. Usikojoe hapa faini laki, Usikojoe hapa ukikutwa utapiga deki, watu hawakujali. Siku moja akachukua chungu kipya akakifunga shanga na vitambaa kama hirizi na kukiweka hapo walipopenda watu kukojoa, na kuweka tangazo.  Tafadhali kojolea kwenye chungu mkojo nauhitaji kwa ajili ya dawa. Watu hawakukojoa tena

MADALALI HII HAIUZWI


KAMATA HUYOOO KAIBA KORODANI

Juzi kati mzee mmoja baada ya kumaliza kumchinja beberu, akachukua korodani na kuamua kuzichoma kwenye moto. Wakati zikiendelea kuiva mbwa koko mmoja hata haijulikani alitokea wapi, akazikwapua na kuanza kutimka nazo. Watoto wa mzee wakaanza kumfukuza mbwa huku wakipiga kelele,'Korodani za baba, mbwa kaiba korodani za baba'. Mzee nae kusikia hayo akajiunga kumfukuza mbwa huku nae akilalamika,'Korodani zangu mbwa anakula korodani zangu'

BAUNSA KALETA BALAA

Baunsa wa night club alienda kutibiwa mgongo kwa doctor.
DOKTA: Ilikuwaje mpaka ukapata mshtuko wa uti wa mgongo?
BAUNSA: Nilipoingia home alfajiri nikitokea kazini,nilisikia makelele
chumbani kwangu nikajua mke wangu yupo na mwanaume
mwingine,nikazama chumbani kwa spidi lakini sikumkuta mtu,mara nikasikia mlango wa sebuleni umefunguliwa kwa fujo,nilipochungulia kupitia
dirishani nikamwona mtu anakimbia huku anavaa shati,nikachukua fridge nikamrushia nikiwa ghorofa ya tatu,hapo ndipo niliposhtua uti wangu wa mgongo.......Alipomaliza tu kauli yake,akaingia mgonjwa mwingine kaharibika kama kagongwa na gari.
DOKTA: Na wewe nini kimekusibu?.
MGONJWA 1: Nilisahau kuweka alarm asubuhi nikachelewa kuamka kwenda
kazini,kazi yenyewe niliajiriwa jana tu baada ya kukaa jobless kwa muda mrefu,nikatoka nje huku navaa nguo,mara nikapondwa na fridge kichwani.......Mara akaingia mgonjwa wa tatu akiwa na hali mbaya kuliko
waliomtangulia.
DOKTA: Na wewe nini tena Yarabi?
MGONJWA 2: 'Doctor,mimi nilikuwa nilitaka kufumaniwa nikajibanza ndani ya fridge,mara ghafla lile fridge likabebwa na kutupwa kutoka ghorofa ya tatu
mpaka chini