HATUPIMI BANDO

26 December 2012

WE ONDOKA ZAKO

Mdada alikuwa anajua kuwa mumewe yuko safari akamkaribisha mpenzi kwake, kwenye saa 6 usiku mumewe akapiga hodi, mdada akamwambia mpenzi simama hapo pembeni jifanye sanamu mengine niachie. Jamaa akasimama kama sanamu mke akamfungulia mumewe na kumpokea mizigo na kumkaribisha ndani. Mume akamuangalia yule jamaa kisha akamuuliza mkewe,' Nini hiki?'. Mke akajibu,' Wamachinga walipita na masanamu wanauza na mimi nikanunua moja'. Mume akajibu ,'OK'. Jamaa akala akalala, kwenye saa 9 usiku akaamka, akaliendea lile sanamu akaliambia,'Pole kwa mbu ndugu yangu, heri uondoke zako mie mwenzio ishu kama hii imenikuta Iringa nikapigwa na baridi siku mbili ndio nikaweza kuondoka. Haya usiku mwema'

No comments: